Ticker

6/recent/ticker-posts

SIKU MOJA TAKRIBANI ASILIMIA 17.13 YA KAYA NCHI NZIMA ZIMESHAHESABIWA

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 Bi. Anne Makinda (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 24,2022 Jijini Dar es Salaam kuhusu Maendeleo ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi. Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 Bi. Anne Makinda akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 24,2022 Jijini Dar es Salaam kuhusu Maendeleo ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

********************

Na Magrethy Katengu

Takribani asilimia 17.13 ya kaya tayari zimeshahesabiwa siku ya Agosti 23 ambapo zoezi hilo linaendelea vizuri huku likivuka lengo ambalo llilowekwa la asilimia 15 ya kaya kuhesabiwa kwa siku moja .

Akizungumza na Waandishi wa habari Kamisaa wa Sensa Spika Mstaafu Anne Makinda amesema kwa mujibu wa Mfumo wa ufuatiliaji na ukusanyaji wa taarifa za Sensa kituo cha kuchakata taarifa za sensa kilichopo Mjini Dodoma kilionyesha asilimia 17.13 za kaya ikiwa ni zaidi ya lengo la asilimia 15 ya lengo lililokadiriwa kufanyika siku ya kwanza hivyo kiwango kimevuka goli licha ya kuwepo changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya maeneo umeme kukatika vishikwambi kukosa charge hivyo makarani kusubiria umeme,kaya moja kuwa na watu wengi lakini wananchi wameonyesha Ushirikiano mzuri .

"Tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa ni matumaini yetu kuwa kasi ya zoezi kuhesabu watu kwa siku zitaendelea kuwa kubwa zaidi hadi kufikia lengo tulilojiwekea kama ilivyopangwa kwani kama alivyoeleza Mhe Rais siyo watu wote wangeweza kuhesabiwa jana hivyo litaendelea kwa muda wa siku saba na ni vyema kwa wananchi kuwa na uvumilivu wa kwamba kila mwananchi ni lazima atahesabiwa"amesema Anna Makinda

Hata hivyo amewasisitiza Wananchi kuhusu maneno mengi mtaani yanayosemwa kuhusu sensa na wakati mwengine inachanganywa sensa na uchaguzi anachotaka kusema ni kwamba hii sensa ni siku saba isilinganishwe na uchaguzi unafanyika siku moja Rais kuitangaza Agost 23 kuwa Siku ya mapumziko ni kuiheshimu tukio kubwa la kitaifa kwani kuiheshimisha kwani zoezi hilo hufanyika kwa mara 10 mara moja.

"Niseme kuwa miaka ya nyuma zoezi hili lilikuwa likifanyika jumapili ya mwishoni mwa mwezi wa nane hivyo madhehebu mbalimbali yakawa yanalalamika tunaingilia siku yao ya ibada tukaona isifanyike siku inayoingiliana na ibada ndiyo maana ikafanyika siku ya Jana"amesema Kamisaa

Hata hivyo amewataka waratibu wa sensa wa Wilaya na Mikoa kugawa fomu ambazo zitajazwa na watu na kuweka namba maalumu ambayo itatumika kwa ajili ya kuweka ahadi kwa watu ambao hawajawahesabu ili kusaidia zoezi kuwa jepesi kwao na kwenda kwa haraka zaidi hivyo wananchi watakapopiga simu zao simu hizo ni bure hazitakuwa na malipo lengo ni kutaja muda watakaokuwepo nyumbani kwao ili wafuatwe kwa lengo la kukamilisha zoezi.

"Niwatake viongozi wa serikali za mitaa kuwaongoza makarani wa Sensa na Kwa kila kiongozi mmoja anatakiwa amuongoze karani mmoja msiwe na shaka mtalipwa kulingana kumuongoza karani kwani posho zenu zipo"amesema Kamisaa

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi Ofisi ya Taifa ya Takwimu Sensa na Makazi ya Watu Amina Msengwe amesema vishkwambi vipo vya kutosha hata kama ikitokea vimepotea au karani ameugua kwa bahati mbaya vipo vya ziada kwa ajili ya kukamilisha zoezi la sensa .

Aidha wito umetolewa Kwa wajumbe wa serikali za mitaa kuongoza na Makarani wa Sensa katika zoezi hilo kwani wao ndiyo wanaofahamu mipaka na watu wao na pesa za malipo yao zipo zilishatengwa .

Post a Comment

0 Comments