Ticker

6/recent/ticker-posts

TCCIA YAJIPANGA KUFANIKISHA MAONYESHO YA BIASHARA MWANZA

Mwenyekiti wa chemba ya wafanyabiashara,Viwanda na Kilimo (TCCIA)Gabriel Kenene akizungumzia na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya maonyesho ya 17 ya wafanyabiashara yanayotarajiwa kufanyika agosti 26 mwaka huu kwenye uwanja wa Nyamagana mkoani Mwanza kulia ni Katibu Mtendaji wa TCCIA Hassan Karambi.

************************

Na SHEILA KATIKULA, MWANZA

WAFANYABIASHARA, wajasiliamali na wawekezaji wameombwa kujitokeza kwa wingi kushiriki maonyesho ya Chemba ya Wafanyabiashara na Kilimo (TCCIA) yanayotarajiwa kuanza Agosti 26 mwaka huu kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa TCCIA mkoa Mwanza, Gabriel Kanene wakati akifanya mahojiani maalum na waandishi wa habari ofisini kwake.

Gabriel amesema zaidi ya nchi nane zinatarajiwa kushiriki kwenye maonyesho ya 17 ya biashara ya Afrika mashariki.

Miongoni mwa nchi zilizothibitisha kushiriki ni pamoja na India, Burundi, Tanzania, Uganda, Kenya, China na Indonesia.

Amesema lengo la maonyesho hayo ni kupanua wigo wa masoko na teknolojia mpya za uzalishaji na kuimarisha uchumi kupitia kilimo na biashara.

Amesema zaidi ya wafanyabiashara 300, makampuni 50 na wageni 250000 kutoka nje ya nchi wanatarajia kushiriki kwenye maonyesho hayo kutokana na kutangazwa kwa royal tuor.

Amesema maonyesho yanajumuisha wafanyabiashara wakati, wadogo na wakubwa, wenye viwanda na wakulima watakaoshiriki maonyesho hayo na kupata fursa mbalimbali ndani na nje ya nchi.

“Tutakuwa na michezo ya watoto, wanyama mbalimbali na tumealika wataalamu kutoka sekta mbalimbali, makampuni na mashirika ili wafanyabiashara waweze kujifunza na kupata elimu ya kujiendeleza kibiashara, kusafirisha bidhaa zao na kupata masoko ndani na nje ya nchi", amesisitiza Kenene.

Post a Comment

0 Comments