Ticker

6/recent/ticker-posts

STAMICO YAJA NA SULUHISHO LA MATUMIZI YA MKAA MBADALA UNAOZALISHWA NA MAKAA YA MAWE

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la STAMICO Dkt Venance Mwase

************

Na Magrethy Katengu

Shirika la Madini Taifa (STAMICO) limesema llitahakikisha linaongeza juhudi kukabiliana changamoto ya mabadiliko ya Tabia nchi inayosababishwa na shughuli za kibinadamu ikiwemo ukataji miti kwa ajili ya matumizi ya mkaa ambao hali hiyo kadri miaka inavyozidi kusongea uoto wa asili umekuwa ikipotea.

Akizungumza na Waandishi wa habari   Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la madini la Taifa (STAMICO ) Dkt Venance Mwasse  amesema Shirika hilo tangu  kuanzishwa kwake   mwaka 1972 na limepitia misukosuko mingi lakini limeendelea kujiendesha na kwa kufanya shughuli zake mbalimbali ikiwemo kufanya tafiti  zinazokwenda  kuleta suluhisho ya changamoto inayoikabili Jamii ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi  inayopelekea uhaba wa  mvua ( ukame).

"Nchi yetu kadri miaka inavyozidi kusogea nayo inakumbana na tatizo la mabadiliko ya tabia nchi hali hii inasababishwa shughuli za kibinadamu ikiwemo ukataji miti kwa matumizi hasa uchomaji mkaaa hivyo STAMICO tumekuja na suluhisho la kubuni mkaa mbadala ujilikanao kwa jina Rafiki BRIQUETTES ubunifu makini suluhisho la nishati mbadala wa utunzaji mazingira ambapo kuna mitambo  ya kutengeneza bidhaa  hiyo  "amesema  Dkt Venance.

Mkurugenzi Venance amesema Shirika hilo katika kipindi cha miaka hamsini lilifanya utafiti huo kwa kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo COSTECH,TIRDO,na Vyuo Vikuu  hivi karibuni   Mkaa abadala uitwa  (Rafiki BRIQUETTES ) ubunifu huo makini suluhisho nishati mbadala ya utunzaji mazingira ambapo tayari utafiti huo ulishakamilika na mtambo wa uzalishaji bidhaa na hiyo  majaribio yalifanyika STAMICO  ikapatiwa cheti na Shirika la viwango Tanzania (TBS) .

Dkt Venance amesema  bidhaa iliyozalishwa iko salama kwa matumizi hivyo amewaasa wananchi waachane na kuharibu mazingira kwa kukata uoto wa asili waanze kutumia bidhaa hiyo kwani nayokwenda kuzinduliwa hivi karibuni.

Hata hivyo amesema ubunifu huo wa mkaa mbadala ni mradi mkubwa unakwenda kuleta suluhisho la mabadiko ya tabia nchi na utafiti huo ulianza 2018 na ulifanyika katika hatua mbalimbali ambapo 2019 matokeo yalionyesha mkaa huo ungenza kutumikia mtumiaji angetakiwa kutumia sufuria mpya na jiko lisingefaa tena huku sufuria ikiharibika yote hivyo wakaona haifai matokeo hayo yanakwenda kuongeza changamoto ya gharama na isingekuwa rafiki kwa watu wenye kipato cha chini ikalazimu kurudi maabara Hadi bidhaa hiyo ilipofaa.

Hata hivyo utengenezaji wa Mkaa huo mbadala wanatumia mabaki ya makaa ya mawe kwa kuchanganya na maranda ya mbao ambapo uzalishaji huo utafanyika katika maeneo ambayo makaa hayo yanapatikana.

 Aidha STAMICO wanatarajia kuiadhimisha miaka hamsini ya Shirika hilo tangu kuanzishwa kwake 1972 na itaafanyika kuanzia Agosti 1-12 mwaka huu  kunafaisha hadi kufikia mwaka huu huku kauli mbiu ikiwa.

 " STAMICO na mazingira kutakuwa  na matukio mbalimbali ikiwemo kupanda miti elfu kumi Dodoma- Ipagala na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira na kugawa misaada kwa wagonjwa wanaogua Saratani pamoja na kugawa Vifaa Kwa watu wenye uziwi watu.

Post a Comment

0 Comments