Ticker

6/recent/ticker-posts

‘TAMISEMI NI MDAU MKUBWA WA TAKWIMU ZA SENSA’ BASHUNGWA


****************

OR- TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amesema TAMISEMI ni mdau mkubwa wa takwimu zitakazokusanywa kwenye Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika tarehe 23 Agosti,2022 ili kuimarisha upelekeaji wa huduma kwa wananchi.

Waziri Bashungwa ameyasema hayo wakati wa mahijiano katika kipindi cha Powerbreakfast cha Clouds Fm mapema leo tarehe 17.08.2022.

Amesema katika upangaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo hususani; upelekaji wa huduma za kijamii na kiuchumi karibu na Wananchi zinahitaji takwimu sahihi ya idadi ya watu ili huduma hizo ziwezi kwenda proportional na idadi ya watu.

‘Huduma hizo ni pamoja na ujenzi wa Vituo vya kutolea huduma za afya kwa maana ya hospitali, vituo cha afya na zahanati, huduma za elimu yaani shule, madarasa, ujenzi wa maabara, mabweni, maabara, miundombinu ya maji pamoja na kufanya msawazo wa watumishi kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa."

Aliongeza: " kwa mfano TAMISEMI inatekeza upatikanaji wa huduma za Afya bure kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano sasa kama hatuna takwimu sahihi hatuwezi kutekeleza jukumu hili ipasavyo na kwa hivyo kuna baadhi ya watoto hawatapata huduma hii kwa sababu tu hawakuhesabiwa na kwenye takwimu zetu hayupo hivyo tunashindwa kumu- accomodate(kumujumuisha)."

Alisema kwa Upangaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo katika Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa (MSM) takwimu zilizokuwa zikitumika ni takwimu ambazo zinapatikana baada ya kufanya makadirio (projection) kwa kutumia Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 kama “base year”.

" Tunatambua kuwa kuna mabadiliko makubwa yametokea katika kipindi cha miaka 10 tangu Sensa ya mwisho ifanyike yaani mwaka 2012 hadi 2022, hivyo Sensa hii itakuwa ni msingi wa kupata takwimu halisi zitakazo akisi mabadiliko hayo, kuwezesha kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo na kufanya maamuzi sahihi kwa maendeleo ya Wananchi wetu kwa kipindi cha miaka 10 au zaidi ijayo."

Mhe. Bashungwa aliwaka Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kutotoka kwenye maeneo yao ya kazi mpaka Sensa ya Watu na Makazi litakapokamilika.

Post a Comment

0 Comments