Ticker

6/recent/ticker-posts

TUSHIRIKI SENSA KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU: MKURUGENZI ZBS


*************

MKURUGENZI wa Taasisi ya Viwango Zanzibar(ZBS) Yusuf Nassor, amesema kuna umuhimu mkubwa wa watanzania kujitokeza na kushiriki zoezi la sensa ili kuiwezesha Serikali kupanga mipango mbalimbali ya kimaendeleo.

Akizungumza kwa nyakati tofauti Nassor amewataka watanzania wote kihakikisha wanaitumia siku ya Agosti 23 kushiriki kikamilifu katima zoezi hilo linalotarajiwa kufanyika nchini kote kutokana na manufaa yake kwa Taifa.

Alisema Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi wana malengo mazuri kwa watanzania hivyo hakuna budi kwa umoja wetu kushiriki katika zoezi hilo la sensa hiyo kwani ni njia mojawapo kuiwezesha Serikali kufikia malengo yake.

"Niwaase viongozi wenzangu kujitokeza kwa wingi na kuwahamasisha wananchi wetu kushiriki sensa kama ambavyo Rais Samia na viongozi wengine wa ngazi za juu wanavyotuhamasisha, kwa pamoja tunaweza kufanikisha hilo" alisema Nassor

Aidha amesema kushiriki katika zoezi hilo kuna faida mbalimbali kwa nchi ikiwa ni pamoja na kuiwezesha Serikali kupanga mipango yake ya kimaendeleo kutokana na idadi ya wananchi wake.

"Tunawaomba wananchi wote bila kujali imani zetu na itikadi zetu ni vyema kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika sensa hii ya watu na makazi, hii itasaidia Serikali yetu kufahamu idadi kamili ya wananchi wake na hivyo kuweka mipango yake ya kuwahudumia" amesema Nassor.

Amesema Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha analiletea Taifa hili maendeleo hivyo hata hatua yake ya kutaka sensa ifanyike amelenga kufahamu idadi ya wananchi wake ili aweke mipango mizuri zaidi hivyo ni vyema akaungwa mkono.

Amesema wao kama viongozi wenye nguvu na hari, wamejiandaa kikamilifu kushiriki katika sensa hiyo wakiamini kuwa kwa kufanya hivyo kutaiwezesha Serikali kuja na mipango sahihi ya kimaendeleo kwa ajili ya wananchi wake hivyo kilichobaki ni kwa wananchi kutumia nafasi hiyo kuhesabiwa.

Aidha katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo amesema tangu Rais Samia aingie madarakani kuiongoza Serikali ya awamu ya sita, ameonyesha dira katika masuala mbalimbali ya kiuchumi na kimaendeleo hali iliyosaidia kuongeza idadi ya wawekezaji kuja kuwekeza nchini jambo ambayo hata Rais wa Zanziar Dk Hussen Ali Mwinyi amekuwa akilifanya

"Leo hii tunaona kwa macho yetu namna idadi kubwa ya watalii wanaoingia nchini, hili limetokana na wazo lake la kuja na filamu ya Royal Tour ambayo kimsingi imeongeza chachu ya watalii kutoka mataifa mbalimbali kuja kuitembelea Tanzania" amesisitiza Mkurugenzi huyo

Amesema ujio wa watalii hao mbali na kuliingizia Taifa fedha za kigeni pia utawafanya waone fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini na kwenda kuzitangaza katika mataifa wanayotoka jambo ambalo litazidi kuineemesha nchi.

Post a Comment

0 Comments