Ticker

6/recent/ticker-posts

TBS KANDA YA KATI YATEKETEZA BIDHAA ZA VYAKULA NA VIPODOZI


GARI likishusha Vipodozi na bidhaa zilizoisha muda wake katika Dampo la Chidaya jijini Dodoma ambavyo vimeteketezwa na Shirika la Viwango (TBS) Kanda ya kati zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 100.


MUONEKANO wa Vipodozi na bidhaa zilizoisha muda vikiwa vimewekwa katika Dampo la Chidaya jijini Dodoma kwa ajili ya kuteketezwa na Shirika la Viwango (TBS) Kanda ya kati zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 100.


Tingatinga likitetekeleza bidhaa katika Dampo la Chidaya jijini Dodoma ambavyo vimeteketezwa na Shirika la Viwango (TBS) Kanda ya kati zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 100.


Mkaguzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Kati Domisiano Rutahala,akizungumza akizungumza na Waandishi wa Habari katika dampo la Chidaya mara baada ya kuteketeza vipodozi na bidhaa za vyakula zilizoisha muda tani 31.2 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 100 leo Agosti 26,2022 jijini Dodoma

...............................


Na Alex Sonna-DODOMA

SHIRIKA la Viwango (TBS) Kanda ya kati limeteketeza Vipodozi na bidhaa za Vyakula zilizoisha Muda tani 31.2 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 100 katika Dampo la Chidaya jijini Dodoma.

Hayo yameelezwa leo Agosti 26,2022 jijini Dodoma na Mkaguzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Kati Domisiano Rutahala wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika dampo la Chidaya ambako ndiko bidhaa hizo na vipodozi vimeteketezwa.

Bidhaa na vipodozi zilizoteketezwa ni kutoka katika Mikoa ya Dodoma,Singida na Tabora na ni kuanzia Novemba 2021 hadi Agosti 2022.

Mtaalamu huyo amesema bidhaa zilizoteketezwa ni zile zilioisha muda pamoja na vipodozi vyenye viambata vya sumu na vilivyoisha muda wake.

“Kwa ujumla bidhaa zote ni tani 31.2 sawa na kilo 3200 zenye thamani ya shilingi milioni 100.9,”amesema Mtaalamu huyo kutoka TBS

Amesema wanateketeza bidhaa hizo kutokana na kuwa na madhara makubwa katika mwili wa mwanadamu.

“Bidhaa za chakula ambazo zimeisha matumizi zina athari kubwa sana mojawapo kutopatikana kwa virutubisho vinavyohitajika pia zinasababisha magonjwa ya muda mrefu na mfupi kama Saratani.

Kwa upande wa vipodozi vinaathari kubwa sana kiuchumi na madhara ya muda mfupi na mrefu kuathiri mifumo ya macho,ukuaji wa watoto na kina mama wajawazito,”amesema Mtaalamu huyo

Hata hivyo anawaasa wafanyabiashara wote kuwa makini kwa kufanya ukaguzi wa bidhaa zao na wajiepushe na uuzaji wa bidhaa zenye viambata vya sumu kwani vina madhara makubwa

Aidha,wanawaomba wazingatie maelekezo ya utunzaji wa bidhaa hizo ili kuendana na uzalisha pamoja na kulinda ubora wake.

Kwa upande wa wananchi,Bw.Rutahala amewaomba waepuke kutumia bidhaa zenye viambata vyenye sumu na kufanya ukaguzi wa kuangalia mwisho wa matumizi ili kuepuka madhara.

“Wafanyabiashara tunapowakamata tuna hatua mbalimbali ambazo huwa tunazichukua zimetaja aina ya faini na hatua za kuchukua,ikiwa ni pamoja na kuzichukua bidhaa hizo na kwenda kuzitekeleteza,”amesema.

Post a Comment

0 Comments