Ticker

6/recent/ticker-posts

WADAU WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KULETA USTAWI WA JAMII

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula, akikata utepe kuashiria kupokea gari aina ya Land Cruser Hard Top kutoka Shirika la Pact Tanzania lenye lengo la kuhakikisha ustawi wa watoto na wazee unaimarishwa nchini, makabadhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma. Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula akiwa ndani ya gari aina ya Land Cruser Hard Top alilokabidhiwa na Shirika la Pact Tanzania, lenye lengo la kuhakikisha ustawi wa watoto na wazee unaimarishwa nchini, makabadhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula, akipokea funguo za gari aina ya Land Cruser Hard Top kutoka kwa kiongozi wa Huduma za Kijamii USAID Tanzania Dkt. Ifeyinwa Udo lenye lengo la kuhakikisha ustawi wa watoto na wazee unaimarishwa nchini, makabadhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Waandamizi kutoka Shirika la Pact Tanzania na USAID mara baada ya kupokea gari aina ya Land Cruser Hard Top lenye lengo la kuhakikisha ustawi wa watoto na wazee unaimarishwa nchini, makabadhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma.

******************************

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMMJW

Na WMJJWM, Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Zainab Chaula ametoa wito kwa wadau kuendelea kushirikiana na Serikali kuwahudumia wananchi hasa katika kuboresha miundombinu na vitendea kazi katika kufikia ustawi wa jamii.

Dkt. Chaula ametoa wito huo leo Agosti 24, 2022 wakati akipokea gari lililotolewa na Shirika la PACT Tanzania kupitia mradi wa Achieve kwa lengo la Wizara kuimarisha Huduma za Ustawi wa jamii hususani uratibu wa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Amesema Serikali inatekeleza majukumu mbalimbali kuhakikisha changamoto katika Jamii zinatatuliwa, hivyo kwa kushirikiana na wadau itaharakisha kufikiwa kwa matokeo tarajiwa.

Ameongeza kuwa wamejadiliana na Shirika hilo katika kuboresha huduma kwa jamii na kuendelea kushirikiana kutekeza miradi na programu mbalimbali hasa katika ustawi wa watoto na wazee ikiwemo afua za malezi makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto na ustawi wa wazee nchini.

"Sisi kama Wizara tunaendelea kutoa wito kwa wadau wengine wajitokeze ili tuunganishe nguvu kwa pamoja kwani tunamsadia Rais Samia Suluhu Hassan kutoa huduma kwa wananchi” alisema Dk. Chaula

Kwa upande wake Mkurugenzi mkazi wa Shirika la PACT Tanzania na mradi wa Achieve Levina Kikoyo amesema lengo hasa la kutoa gari hilo ni kuhakikisha mifumo ya Serikali inafanya kazi katika utekelezaji wa program na huduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali ili zinawafikia walengwa kwa ustawi na maendeleo ya jamii.

"Tumefanya kazi na Wizara hii kwa sababu katika Huduma zetu tunafanya kazi ya kuwafikia watoto zaidi ya 600 nchini walio katika mazingira hatarishi hasa katika maambukizi ya VVU, lengo kuhakikisha watoto wanatambuliwa, wanapata Huduma stahiki na kufubaza VVU" alisema Levina

Post a Comment

0 Comments