Ticker

6/recent/ticker-posts

JAJI WARIOBA ASHUSHA NYUNDO NZITO KWA VIONGOZI WA DINI NA NA WA KISIASA

Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba akizungumza katika katika semina elekezi iliyoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere ya wajibu wa pamoja wa wadau katika kulinda kushirikisha Mfumo wa Demokrasia ya vyama vingi iliyofanyika leo Septemba 20,2022 Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mzee Joseph Butiku akizungumza katika katika semina elekezi iliyoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere ya wajibu wa pamoja wa wadau katika kulinda kushirikisha Mfumo wa Demokrasia ya vyama vingi iliyofanyika leo Septemba 20,2022 Jijini Dar es Salaam

*********************

Na Magrethy Katengu


Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba amewashauri Viongozi wa dini,siasa,kutumia wadhifa walionao kuondoa,ubaguzi wa kisiasa,kidini,kikabila ili kusaidia kujenga Taifa lenye umoja na mshikamano kimaendeleo.

Ushauri huo ameutoa leo Jijini Dar es salaam katika semina elekezi iliyoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere ya wajibu wa pamoja wa wadau katika kulinda kushirikisha Mfumo wa Demokrasia ya vyama vingi ambapo amesema miongoni mwa jamii zetu bado kuna kasumba ya kubaguana hali itakayoleta migongano hivyo lazima ichukuliwe tahadhari mapema .

"Takribani ni miaka thelathini mfumo wa vyama vingi kuanzishwa lakini nimekuwa nikiangalia mwenendo wa nchi hii bado kuna baadhi ya viongozi wamekuwa wakitumia wadhifa wao vibaya kuharibu Demokrasia vibaya kutoa maneno mazito yanayoashiria uvunjifu umoja na mshikamano "amesema Warioba.

Sanjari na hayo Jaji Warioba amesema ifike wakati chaguzi zetu zikazp kuwe na mabadiliko makubwa mfumo wa vyama vingi ufanyike bila kuwepo na udikteta ubaguzi na unyanyasaji wa vyama vya kisiasa hadi kupelekea wengine kuhama nchi kuelekea nchi jirani lakini sasa wamerudi kuijenga nchi.

Hata hivyo amesema baadhi ya wanasiasa kutumia madhabahu ya nyumba za ibada kuongelea Siasa na kitendo hiki kikiendelea kitasababisha kuleta ubaguzi baina ya watu hivyo sheria kali iwekee kuzuia watu kuigia katika nyumba za ibada watu muelekei wao uwe ibada siyo Siasa.

Kwa upande wake aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha NSSR Mageuzi James Mbatia amesema Viongozi wa Siasa nchini wamekuwa hawaelewani ukiangalia chuki imewajaa mioyoni hivyo ifike wakati Tanzania yetu ibadilike kifikra kukaa kwa pamoja kusuluhisha madhaifu yao ...

"Tumekosa hali ya kukaa pamoja kusikilizana na kujenga fikra ya kusaidia Siasa tunazozipenda zisiwe za chuki zinazosababisha uchochezi kwani haitasaidia chochote tunatakiwa kujenga Tanzania yenye mtazamo chanya iliyo na misingi bora ya kidemokrasia inayojenga Taifa imara kiuchumi"amesema Mbatia

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Tanzania Bara Mh. Christina Mdeme alisema kupitia semina hiyo tutapata uwelewa Mambo mbalimbali kwani kuna mawazo mbalimbali namna gani swala la umoja,amani na maendeleo linasimamiwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere takribani miaka 25 tangu kuanzishwa.

"Sisi sote tinaamini kwamba Nchi yetu ya Tanzania ambayo imepiga hatua kubwa sana katika swala la umoja,amani, maendeleo na hivo kuwa kioo na walimu wa Nchi zingine" alisema Mdeme.

Aidha Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mzee Joseph Butiku alisema Viongozi wote hawana budi kuakisi yaliyofanywa na Waasisi wa Taifa hili hayati Mwalimu Juliusi Kambarage Nyerere na Amani Abeid Karume kuweka misingi imara ya Amani,Umoja na Mshikamano na kuunda taasisi hiyo na Sasa inatimiza miaka 25 kuwapa mwelekeo mzuri .

Post a Comment

0 Comments