Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMATI YA AMANI YA MKOA WA DAR ES SALAAM YATOA TAMKO KUHUSU PANYA ROAD ,



*****************************

Na Magrethy Katengu

Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam imewasisitiza wazazi,walezi kuhakikisha wanakuwa karibu na watoto wao kwa kuwapatia malezi bora Ili kusaidia kuepukana na vitendo makundi ya ushawishi kutenda matukio ya kihalifu ikiwemo wizi,ubakaji,kwani Sasa imekuwa tushio kubwa .

Wito huo ameutoa leo Jijini Dar es salaam Afisa Mahusiano na Umma wa kamati ya Amani Dkt. Catherin Yatosha wakati akitoa tamko la kamati hiyo ikiwa ni Muendelezo wa Maadhimisho ya siku ya amani Duniani ambapo ameitaka Jamii kuendelea kuilinda na kuidumiaha Amani kwa kuendelea na udhibiti wa vijana wahalifu wanaojaribu kuvuruga utulivu uliopo Kwa kufanya vitendo viovu vya kusikitisha hivyo amewasihi vijana wengine wanaojihusisha na panya road kuacha mara moja.

"Amani na utulivu tulio nao tuudumishe hivyo kamati ya amani tunaungana na Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha vitendo hivi vya viashiria vya uvunjifu wa amani vinatokomezwa mara moja kwani imetusikitisha sana kuona baadhi ya ndugu zetu wanakatishwa uhai wao"amesema Dkt Yatosha.

Aidha Dkt Yatosha alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa Wazazi kufuatilia mienendo na malezi ya watoto wao ili kuwaepusha vijana wao kujiunga na vikundi vya kihalifu ikiwemo panyaroad .

Naye Mjumbe wa Kamati ya Amani ya Mkoa huo Athuman Mlimasunzi ametoa rai kwa watanzania wote kuwaunga Mkono viongozi wa Kitaifa na viongozi wa dini katika kudumisha amani siyo kutumia majina yao na kuwachafua hivyo amewaomba waliotumia mitandao ya Kijamii kumchafua Shekhe waache na waombe radhi .

Post a Comment

0 Comments