Ticker

6/recent/ticker-posts

TANTRADE YAWAUNGANISHA WAFANYABIASHARA WA TANZANIA NA WAFANYABIASHARA KUTOKA NCHINI INDIA


***************

Ujumbe wa wafanyabiashara 15 kutoka Nchini India umekutana leo tarehe 22 Septemba, 2022 na Wafanyabiashara wa Tanzania wa sekta zaidi ya 10 kwenye Ukumbi wa Sabasaba kwenye Uwanja wa Maonesho wa Mwl.J.K. Nyerere (Sabasaba) Jijini Dar Es Salaam.

Mkutano huo ulioandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini Tanzania(TanTrade) kwa Kushirikiana(ITTC) umelenga kuunganisha Wafanyabiashara wa ndani na wa nje ili kukuza soko la bidhaa za ndani kwa kufanya mazungumzo ya ana kwa ana (B2B)

Katika mkutano huo Wafanyabiashara zaidi ya 15 kutoka India walikutanishwa na Wafanyabiashara zaidi ya 140 katika sekta za korosho, nafaka, kahawa, Kunde, Ngano, Parachichi, Samaki na Mazao ya Bahari, Miliki na Makazi, Vifungashio, malighafi za Plastiki, Pembejeo za Kilimo na Magari ya Umeme.

Akizungumza baada ya mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi Latifa Khamis amesema kuwa mkutano huo utaibua fursa mbalimbali za and Uwekezaji na Biashara ambapo TanTrade itatoa tathimini ya mafanikio ya mkutano huo.

" Tunaamini kwamba baada ya hapa kuna fursa ambazo zitapatikana hatimaye tutaweza kuzikusanya na kutoa tathmini yake katika siku za usoni "

Kwa upandewake kiongozi wa ujumbe huo kutoka Nchini India Dkt. J. Shrenk Nahar amesema kuwa wanategemea kupata bidhaa bora ambazo zitachochea mzunguko mkubwa wa kibiashara baina ya Wafanyabiashara.

Ameongeza kuwa tayari kuna bidhaa tatu ikiwemo zao la korosho, ambazo wamevutiwa nazo na wangependa kusaini makubaliano na Wafanyabiashara kwa hatua nyingine za kibiashara.

Katika mkutano huo baadhi ya kampuni zimeafanya makubaliano ya awali ya kuwa na soko endelevu ikiwa ni pamoja na korosho zilizobanguliwa zaidi ya Tani 2000 , Korosho ghafi tani 100 kila mwezi, Biashara ya Ngano, majadiliano ya Nano-Urea, fursa za wakala wa magari na pikipiki zinazotumia Umeme na Uendelezaji wa Miliki na Makazi.

Post a Comment

0 Comments