Ticker

6/recent/ticker-posts

KARIA AMPONGEZA MKURUGENZI WA SHULE ZA ALLIANCE KWA KUFANIKISHA MASHINDANO YA LIGI YA MABINGWA WA MKOA

Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini Wallace Karia akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa ligi hiyo.
Wachezaji wa timu ya Bunda queens wakishangilia baada kuwa washindi wa kwanza kwenye mashindano ya ligi ya mabingwa wa mikoa wanawake(WRCL2022) yaliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya Alliance iliyopo Kata ya Mahina mkoani Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima akimkabidhi kombe mchezaji wa timu ya Bunda Queens baada ya kupata ushindi.


*******************

Sheila Katikula,Mwanza

Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini,Wallace Karia amempongeza Mkurugenzi wa shule za Alliance zilizopo mkoani Mwanza James Bwire kwa kusaidia kufanikisha mashindano ya ligi ya mabingwa wa mikoa wanawake 2022.

Hayo yamesemwa jana mara baada ya kumalizika kwa ligi hiyo iliyoshirikisha timu 18 kutoka mikoa mbalimbali nchini, iliyofanyika kwenye uwanja wa shule za Alliance zilizopo Kata ya Mahina mkoani hapa.

Amesema michuano hiyo imefanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania na imepata mwitikio kwa sababu timu zimejitikeza kwa wingi.

"Timu zimejitikeza kwa wingi kushiriki kwa sababu ya maandalizi mazuri yaliyofangwa na waandaaji TFF na uongozi wa shule ya Alliance kusaidia ligi hii.

Hata hivyo ameongeza kuwa Shirikisho la mpira wa miguu litaendelea kusaidia wawekezaji wa ndani ambao wana vituo vya kulelea vipaji vya soka kuanzia ngazi ya chini.

"Tutaendelea kusaidia wawekezaji wa vituo vya kulelea vipaji kama Alliance na Fountain Gate kwa sababu wanafanya kazi nzuri ya kuibua vipaji kuanzia chini na kupelekea kupata wachezaji bora.

"Tutaendelea kuwaongezea nguvu wamiliki wa vituo hivi katika kuwapa nafasi ya kuandaa michuano mbalimbali ya ligi daraja la kwanza itafanyika katika kituo Cha Fountain Gate Dodoma na ligi ya mabingwa wanawake ambayo itafanyika kwenye Viwanja vya Alliance,"amesema Karia.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima amewapongeza Mkurugenzi wa shule za Alliance pamoja na waandaaji wa ligi hiyo kwa kufanya maandalizi mazuri.

Amesema ni vema kandaaa vipaji kuanzia chini ili kuweza kupata wachezaji bora kwani mpira siyo ajali unahitaji maandalizi.

Ligi hiyo imemalizika huku timu ya Bunda Queens ikijinyakulia ubingwa baada ya kuifunga Mwanza Queens kwa penalti 5-4 baada ya kutoka sare dakika 90, na mshindi wa tatu ni Jmk Parks na nne ni Geita Queens.

Post a Comment

0 Comments