Ticker

6/recent/ticker-posts

MATAIFA 13 YASHIRIKI MASHINDANO YA GOFU YA DIPLOMATIC


Mashindano ya mchezo wa gofu maarufu kama Diplomat Tournament yamemalizika kwa kishindo yakiwa yamehudhuriwa na wachezaji 140 kutoka mataifa 13.

Mashindano hayo yaliyochezwa kwa siku 2 katika viwanja vya Kili Golf Jijini Arusha yalifungwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe.Nape Nnauye ambaye aliwahamasisha wazazi kuwaruhusu watoto wao kushiriki katika michezo.

Waziri Nape ambaye pia ni mchezaji wa mchezo huo ambapo aliweza kucheza mashimo 27 aliwasihi Watanzania kupenda mchezo huo na waondokane na dhana kuwa mchezo huo ni wa matajiri peke yake.

Kwa upande wake mwanzilishi wa mashindano hayo ya Gofu ya Dilpomatic ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuwa mashindano hayo yamekuwa ni chachu ya kuongeza watalii wa michezo kuja kutembelea Tanzania.

“Kuna ambao wanakuja kwa ajili ya kushiriki mashindano haya lakini wakimaliza wanapenda kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo Arusha,” amesema Waziri Ndumbaro.

Amesema kuwa licha ya kuongeza watalii, mashindano hayo pia yamekuwa yakitoa ajira kwa vijana wasaidizi wa wachezaji ( Caddie) pindi wanapokuwa katika mashindano.

Post a Comment

0 Comments