Ticker

6/recent/ticker-posts

MRADI BOMBA LA MAFUTA MBIONI KUANZA, FURSA ZATAJWA KWA WAFANYABIASHARA.

Mkuu wa Mkoa Mgumba wa pili kushoto akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa Pili Mnyema pamoja na mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa wakwanza kulia na wakwanza kushoto ni Mratibu wa mradi wa Bomba la mafuta.
Wafanyabiashara wa Mkoa wa Tanga wakifuatilia hotuba ya mkuu wa Mkoa wa Tanga Omary Mgumba kabla ya kufungua kikao hicho.


**************************

Na Hamida Kamchalla, TANGA.

SERIKALI haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wale wote ambao wenye nia ovu ya kutaka kuichafua taswira ya nchi kupitia ujenzi wa mradi mkubwa wa bomba la mafuta kwani Mkoa umejikita katika kuhamasisha na kulinda amani.


Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa Mkoa wa Tanga Omary Mgumba wakati akifungua kikao cha pili cha kutangaza fursa zilizopo katika mradi huo ambapo Wakandarasi waliopata nafasi katika utekelezaji mradi kuwatangazia fursa wafanyabiashara wa Mkoa wa Tanga.


Amesema Mkoa umejikita katika kuhamasisha ubora na viwango ili kuongeza uaminifu na uadilifu kwa watoa huduma, na kwamba atakayebainika kutoa huduma zilizo chini ya viwango serikali haitamvumilia.


"Hata hivyo serikali haitasita kuchukua hatua za kisheria na kwa mujibu wa mkataba, kwa muhusika yeyote atakayetaka kuichafua taswira ya Mkoa, na nchi kwa ujumla kwa kutoa huduma zilizo chini ya viwango tulivyokubaliana" amesema Mgumba.


Aidha Mgumba amebainisha kwamba wakandarasi wanaotoka katika Mataifa mengine kuja kutekeleza mradi huo hawana budi kufuata sheria, taratibu na kanuni kwa mujibu wa sheria zilizopo katika mikataba yao.


"Mmekuja kwa kupata fursa ya kujenga mradi huu, ni vizuri lakini wajibu wenu ni kutoa nafasi za ajira kwa Watanzania kwenye zile kazi ambazo hazihitajiki utaalamu mkubwa mpaka wa kutoka nje, haiwezekani kila kitu kuwepo nchini halafu muagize watu au vitu kutoka nje" amesema.


Aidha amewataka wamiliki wa Kampuni za ndani kuchangamkia fursa katika kuendesha mnyororo wa thamani na kujiletea maslahi ya Taifa kwa kutetea fedha kutoka nje nchi na kufanya mradi huo kutokuwa na manufaa kwa wananchi kama inavyoelezwa.


"Kampuni za ndani naona mpo wengi mmealikwa hapa, tuchangamkie fursa na tushiriki kikamilifu kwenye mnyororo mzima wa thamani, angalau miaka mitatu ya mradi fedha zibaki hapa hapa, siyo tunafanya kazi Tanzania fedha zinakwenda Mataifa mengine" amesema.


"Mradi huu ukitekelezwa, naamini kwa mujibu wa sheria utaacha wataalamu wengi wenyeji, kwahiyo uhamishaji wa tekinolojia ukatekelezwe kwelikweli, mkawe wawazi hasa kwa Yale makampuni ya wakandarasi kutoka nje na tekinolojia yao ambayo sisi hatuna" amesisitiza


Hata hivyo Mgumba amewataka wananchi waliopo katika maeneo ya jirani kukulinda mradi huo kwa kutoa taarifa serikalini mara tu wanapoona dalili za uhalifu kwa vipindi vyote ambapo utekelezaji utakuwa ukiendelea.


"Mradi huu ni wa Watanzania, nitoe wito kwa wanaotafita ajira, vibarua kwa kada zote katika fursa zimeshaoatikana katika mradi huu, ziwe za kibiashara na huduma, muweze kuzichangamkia fursa hizi kuanzia sasa mpaka pale zitakapotangazwa na kuendelea" amesema.


"Lakini pia kwa wale waliopitiwa na mradi huu katika sehemu zote hususani kwa mkoa wa Tanga kukulinda kabla, wakati na baada ya ujenzi, kwa hujuma au tishio lolote lile mtalolisikia, ni vizuri mkatoa taarifa kwa serikali na utekelezaji wa mradi kwa taarifa yoyote, kwasababu walinzi wa mradi huu ni sisi Watanzania" amesema.

Post a Comment

0 Comments