Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA ASHIRIKI MAZISHI YA MALIKIA ELIZABETH II


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Muwakilishi wa Mfalme Charles III, Cynthia Gresham wa Uingereza pamoja na Balozi wa Tanzania nchini humo Dkt. Asha-Rose Migiro mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Luton tarehe 17 Septemba, 2022 kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth II wa Uingereza yatakayofanyika tarehe 19 Septemba, 2022 Jijini London.

*************************

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili jijini London, Uingereza kwa ajili ya kushiriki shughuli rasmi ya msiba wa Malkia Elizabeth II.

Siku ya Jumapili, viongozi mbalimbali walioalikwa akiwemo Rais Samia watatoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu kwenye eneo la Westminster Hall ambapo pia atatia saini kitabu cha maombolezo.

Baada ya hatua hiyo Rais Samia atahudhuria hafla fupi ilioandaliwa na aliyetamkwa kuwa Mfalme Charles III ambaye amemrithi mama yake Marehemu Malkia Elizabeth II.

Hafla hiyo ambayo pia imeandaliwa na Malkia Mfariji (Queen Consort), Camilla Parker Bowles itafanyika katika Kasri ya Buckingham jijini London.

Aidha, siku ya Jumatatu, Rais Samia atahudhuria Mazishi ya Kitaifa ya Malkia Elizabeth II yatakayofanyika kwenye Kanisa la Westminster Abbey. Mwili wa Malkia Elizabeth utalazwa kwenye kasri la Windsor.

Post a Comment

0 Comments