Ticker

6/recent/ticker-posts

TATIZO LA AFYA YA AKILI CHANZO CHA VITENDO VYA UKATILI

Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dk. Nandera Mhando akifungua kongamano la tisa la kutoa matokeo ya utafiti lilioandaliwa na Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) na Hospital ya Taifa Muhimbili.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) Prof.Bruno Sunguya akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano la Tisa la kutoa matokeo ya Utafiti lilioandaliwa na Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) na Hospital ya Taifa Muhimbili.

********************

Na Magrethy Katengu

Licha ya Jitihada zinazofanywa kuhakikisha vitendo vya ukatili vinapungua lakini hali bado inazidi kuwa mbaya huku chanzo kinachosababisha ni Mtu kuwa na tatizo la afya ya akili hali inayosababishwa kufanya matukio ikiwemo kubaka,kulawiti,kuua,kupiga, hivyo Jamii haina budi kutoa taarifa wanapoona kiashiria kwa mtu yeyote.

Akizungumza Jijini Dar es salaam Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Nandera Mhando katika uzinduzi wa Kongamano la tisa la Kisayansi kuhusu Magonjwa ya afya ya akili na ukatili lililoandaliwa na Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) na Hospital ya Taifa Muhimbili amesema kuwa bado katika Jamii kuna ongezeko kubwa la vitendo vya ukatili wa kijinsia na wanaofanya vitendo hivyo baadhi yao wanaonekana wana akili timamu kumbe wana tatizo la afya ya kiakili na vitendo hivyo mhusika wa hutenda kutokana kushindwa kufikiria kabla na hata kuomba ushauri .

"Sononeko,mawazo yaliopitiliza upweke ni hali ambayo anakuwa nayo mtu hasa anapokutwa na Jambo ambalo anashindwa kufikiria namna ya kulitatua mfano baba anaambiwa na mama mtoto unayemuona hapa siyo wako hivyo mzazi huyo wa kiume anaingia katika hali ya kuwa na mawazo yaliyokithiri na kushindwa kujizuia kuchukua maamuzi kuua mtoto na mama na yeye mwenyewe hivyo katika Jamii nyingi na vitendo vya mauaji Jamii tunapoona viashiria tutoe taarifa mapema Ili kuzuia ". Amesema Dkt.Mhando

Naye Mtafiti wa afya ya akili Daktari Samweli Likindikoki amesema tafiti wanazofanya inaonyesha ukatili dhidi ya wanawake,watoto unasababishwa na afya ya akili unatakiwa kushughulikia changamoto vipigo,ulawiti,kubakwa na inakuwa na madhara makubwa kama haiticgukuliwa hatua ikiwemo sononeko mawazo hali ni hali ya hatari kama isipochuliwa tahadhari mapema kiafya hivyo bora ya kuondoa hii changamoto ya sonona kiwewe hofu.

Naye Mtafiti kutoka Chuo Cha Muhasi Daktari Jessie Mbwambo amesema kuwa kupitia kongamano hilo lililowasogeza watafiti pamoja kubadilishana mawazo kuhusu changamoto zinazojitokeza kwenye Jamii na chanzo chake husababishwa na afya ya akili kwani tafiti zao wamekutana na baadhi ya watoto waliojaribu kujiua wakaongea nao kuwabadilisha akili zao na mpaka leo wanaendelea na maisha hivyo anasema suala hili Jamii ikipatiwa elimu ya kutosha namna ya kukabiliana na msongo wa mawazo inaweza kusaidia kupunguza vitendo vya ukatili.

Aidha amesema baadhi ya watu wanaowahudumia wengine hukutana na majanga makubwa ikiwemo ajali,madeni hivyo hukosa usingizi hupungua uzito na kupoteza uwezo wa kufanya maamuzi huona maisha hayaendi hivyo wao kama Madaktari hutumia njia nyingi kuwasaidia hivyo ameishauri Jamii afya ya akili inaweza kumpata mtu yeyote na inasaidika na kupatiwa ufumbuzi kabla ya kutokea madhara.

Post a Comment

0 Comments