Ticker

6/recent/ticker-posts

UJENZI WA MIRADI YA MAENDELEO HALMASHAURI YA IKUNGI YASHIKA KASI

Muonekano wa baadhi ya majengo ya Kituo cha Afya cha Kata ya Ntuntu ambayo yanaendelea kujengwa. 

 

Na Suzan  Kajinga, Ikungi DC


HALMASHAURI ya Wilaya Ikungi mkoani Singida inaendelea kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwepo ya ujenzi wa vitu vya afya.

Moja ya ujenzi unaotekelezwa kwa kasi ni wa Kituo Cha Afya Kata ya Ntuntu ambao umepiga hatua kubwa ambapo Jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD), Maabara na kichomea taka ujenzi wake umefikia asilimia 80.

Majengo mengine yanayoendelea kujengwa ni Jengo la Mama na Mtoto ambalo limefikia  hatua ya nguzo mlalo (Linta) na Jengo la kufulia ambalo lipo katika hatua  ya ukamilikaji huku Jengo la Upasuaji likiwa kwenye hatua ya upauaji.

Hatua hiyo nzuri ya ujenzi wa kitu hicho cha afya umefikiwa na usimamizi mzuri wa ujenzi wa halmashauri hiyo chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Justice Kijazi, Mkuu wa Wilaya, Mbunge, Diwani, Wananchi pamoja na Wataalam mbalimbali ikiwepo na Mkandarasi. 

Post a Comment

0 Comments