Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI UMMU;UVAAJI BARAKOA SIYO LAZIMA KUJIKINGA NA UVIKO-19



************************

Na Magrethy Katengu

Serikali ya Tanzania imepunguza masharti ya kujikinga na Ugonjwa wa Uviko 19 ikwemo kuondoa ulazima wa kuvaa barakoa isipokuwa pale inapobidi, baada ya nchi kufikia asilimia 60 ya walengwa wa chanjo ya Uviko 19.

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema licha kupunguzwa kwa masharti hayo Serikali inahimiza Wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya Ugonjwa wa Uviko 19 kunawa mikono Kwa maji tiririka na sabuni kutumia vipukusi kujikinga na magonjwa mengine ya kuambukiza ikiwemo kuhara,kipindupindu.

"Toka kutangaza kwa uwepo wa Uviko-19 nchini mwezi Machi 2020 mpaka kufikia 7Septemba 2022 Tanzania tumeshuhudia jumla ya visa 35,747 vilivyothibitishwa vya maambukizi ya Uvico-19 na vifaa 808"amesema Waziri Ummy

Hata hivyo uchambuzi katika Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na vituo vya kutolea huduma za afya 7Septemba mwaka huu imeonesha kuwa kati ya watu 289 ya waliopimwa watu 23 wamethibitishwa kuwa na maambukizi ya Uviko-19 huku wagonjwa 7 walilazwa wodini na wote hawajapata chanjo ya ugonjwa huo na mgonjwa mmoja anatumia hewa tiba ya Oksijeni hivyo ugonjwa bado nchini .

Sanjari na hayo Serikali inaendelea kufanya uchunguzi wa afya dhidi ya magonjwa ya milipuko kwa wasafiri wa kimataifa katika Viwanja vya ndege vya kimataifa,bandarini na mipaka ya nchi kavu kufanya vipimo vya vipima joto (thermoscans) huku kusitisha kufanya kipimo cha haraka (Rapid Test) kwa wasafiri wanaotoka nchi zote wenye vyeti vya chanjo Uviko-19 au cheti Cha TT-PCR .

Sambamba na hayo Serikali imeongeza umri wa watoto kutoka nje ya nchi wanayotakiwa kusamehewa kupima Uviko-19 kabla hawajaingia nchini kutoka umri wa miaka 5 ilivyokuwa awali Hadi miaka 12.

Aidha Waziri Ummy ameshukuru wanahabari wote ,wadau wa Maendeleo wakiwemo WHO,UNICEF,USAID,CDC,GAV na mashirika yasiyo ya kiserikali Kwa mchango wao mkubwa wa mapambano dhidi ya Uviko-19.

Post a Comment

0 Comments