Ticker

6/recent/ticker-posts

VIJANA JKT MARAMBA WAPEWA SOMO BAADA YA KUHITIMU MAFUNZO.

Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Surumbu akikagua gwaride la wahitimu wa mafunzo ya awali ya jeshi la kujenga Taifa, JKT Maramba, operesheni Jenerali Venance Mabeyo 2022.
Wahitimu wa mafunzo ya awali ya kijeshi wakiwa katika gwaride.
Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Surumbu akitoa hotuba.
Mwakilishi wa mkuu wa JKT, Kanali Aisha Matanza akitoa hotuba kwa wahitimu.

Wahitimu wakimsikiliza mkuu wa Wilaya akitoa hotuba yake kabla ya kufungua mafunzo.


********************

Na Hamida Kamchalla, MKINGA.


VIJANA waliopata mafunzo ya kijeshi wameshauriwa kuyatumia kwa àjili ya kudumisha amani na uzalendo kwa nchi yao badala ya kuyatumia katika kujiingiza kwenye vitendo vitakavyo hatarisha usalama wa nchi.


Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Mkinga Kanal Maulid Surumbu wakati wa ufungaji wa mafunzo ya awali ya kijeshi oparesheni Venance Mabeyo yaliyofanyika katika kikosi na 838 KJ Maramba JKT wilayani Mkinga mkoani Tanga.


Alisema kuwa serikali inafanya uwekezaji mkubwa Ili kuhakikisha vijana wanashiriki mafunzo wanaweza kuwa na tija ikiwemo kuleta mabadiliko makubwa kwenye jamii husika na kuwa sehemu ya mchango katika kujiletea maendeleo.


"Taifa linamatarajio makubwa kwenye ndio maana mmeweza kufika hapa na kupata mafunzo hivyo niwaase mtumie mafunzo mliyoyapata kudumisha uzalendo na moyo wa kuipenda nchi yenu na kujiepusha na vitendo viovu"alisema Kanali Surumbu.


Hata hivyo aliwataka vijana hao kudumisha umoja na nidhamu Ili iwasaidie katika kutokomeaa vitendo viovu kama uhalifu na mambo ambayo yanakwenda kinyume na kiapo chao


Nae Mwakilishi wa Mkuu wa jeshi la kujenga Taifa Kanal Aisha Matanza alisema kuwa majukumu ya jeshi hilo ni pamoja na malezi kwa vijana, uzalishaji Mali sambamba na uzalendo kwa Taifa lao.


Hivyo alisema kuwa kupitia mafunzo hayo vijana wanaweza kufundishwa kuwa wakakamavu nawajasiri hivyo ni Imani ya jeshi mafunzo hayo wataweza kuyatumia katika kutatua changamoto za kimaisha bila ya kuvunja Sheria.


"Nidhamu iwe ni silaha katika jukumu lolote mtakalokuwa mkilitekeleza hivyo ni dhamira ya serikali ni kuona mafunzo hayo yanakuwa sehumu ya chachu ya mabadiliko Kwa vijana Kwa kutumika katika misingi sahihi"alisema Kanal Matanza.


Nao wahitimu wa mafunzo hayo waliishukuru serikali kwa kuwapatia mafunzo hayo kwani yamewasaidia kuwajengea ukakamavu na ujasiri ikiwemo uzalendo kwa nchi yao.


Mmoja wa wahitimu hao Agness Massawe alisema "licha ya kujifunza mafunzo ya kijeshi lakini pia tumeweza kujifunza mbinu mbalimbali za uzalishaji mali, kulima ufugaji pamoja na ufundi stadi".

Post a Comment

0 Comments