Ticker

6/recent/ticker-posts

DKT. TAX AWATAKA WATUMISHI KUCHAPA KAZI KWA BIDII NA KUSHIRIKIANA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwa amepokea shada la maua kutoka kwa Bi. Theresia Msendo mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma. Anayeshuhudia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine alipowasili katika Ofisi za Wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz alipowasili katika Ofisi za Wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (kulia) akizungumza katika kikao cha katika kikao cha makabidhiano ya Ofisi kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (hawapo pichani) kilichofanyika Mtumba jijini Dodoma

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza katika kikao cha makabidhiano ya Ofisi kati yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax kilichofanyika Mtumba jijini Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza katika kikao cha makabidhiano ya Ofisi kati yake na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula kilichofanyika mtumba jijini Dodoma

Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Alex Mfungo akizungumza katika kikao cha makabidhiano ya Ofisi kati ya Mhe. Dkt. Tax na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mulamula kilichofanyika Mtumba jijini Dodoma
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akikibidhi rasmi Ofisi kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika Ofisi za Wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar Bi Mariam Haji Mrisho akitoa neno la shukurani katika hafla ya Makabidhino ya Ofisi kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax iliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma
Baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara wakifuatilia hafla ya Makabidhino ya Ofisi kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax na mtangulizi wake Balozi Mulamula (hawapo pichani) iliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma
Sehemu nyingine ya Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara wakifuatilia hafla ya Makabidhino ya Ofisi kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na mtangulizi wake Balozi Mulamula (hawapo pichani) iliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na mtangulizi wake Balozi Mulamula wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara baada ya kukamilika kwa hafla ya Makabidhino ya Ofisi iliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na mtangulizi wake Balozi Mulamula katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara baada ya kukamilika kwa hafla ya Makabidhino ya Ofisi iliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma


****************************

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax amewataka watumishi wa Wizara kuendelea kuchapa kazi kwa bidii, ufanisi na kushirikiana ili kufikia matarajio ya serikali na wananchi kwa ujumla.


Dkt. Tax ametoa rai hiyo leo katika Ofisi za Wizara Jijini Dodoma mara baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula.


Dkt. Tax amesema watumishi wa Wizara wanatakiwa kuhakikisha wanatumia weledi na kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu ya Wizara ili kuleta tija na ufanisi wakati wote.


“Sisi ni timu ya ushindi, tuendelee kuchapa kazi, nitashirikiana na watumishi wote wa Wizara, kuhakikisha tunatekeleza majukumu yetu kwa viwango na kwa muda sahihi, tuwe wabunifu na tujitahidi kufanya kazi kama timu ili kufikia matarajio ya Serikali yetu na wananchi wote kwa ujumla,” alisema Dkt. Tax


Ameongeza kuwa kazi ya kukuza uhusiano kati ya Tanzania na nchi mbalimbali, Jumuiya za kikanda na kimataifa haiwezi kufanikiwa ikiwa watumishi hawatashirikiana na kufanya kazi kwa pamoja kama timu huku wakizingatia weledi, uzalendo na ubunifu kwa maslahi mapana ya taifa.


Akizungumza katika makabidhiano hayo, Balozi Liberata Mulamula amewashukuru Watumishi wa Wizara kwa ushirikiano waliompatia alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambao ulimuwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.


“Nimeacha timu imara nawashukuru wote kwa ushirikiano mlionipatia na niwaombe muendelee na moyo huohuo katika kufanikisha majukumu ya wizara,” alisema Balozi Mulamula.


Awali akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbrouk Nassor Mbarouk amemshukuru Balozi Mulamula kwa ushirikiano aliompatia katika kipindi chake na kumsihi aendelee kushirikiana nao kwa kuzingatia hazina kubwa ya uzoefu na ujuzi alionao katika sekta ya mambo ya nje.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine alisema Wizara imeendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kumuahidi Dkt. Tax kuwa watumishi wako imara na wataendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni na hivyo kuleta tija kwa wizara na taifa kwa ujumla

Post a Comment

0 Comments