Ticker

6/recent/ticker-posts

IGP WAMBURA ATAKA MABADILIKO YA KIUTENDAJI


*************************

07/10/2022 DODOMA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura ametaka mabadiliko ya kiutendaji kwa maafisa na askari wa Jeshi hilo kwa kufanya kazi kwa weledi na kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kulinda usalama wa raia na mali zao.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, Kamishna wa Menejimenti na Rasilimali Watu CP Benedict Wakulyamba wakati akifunga Warsha ya kuwajengea uwezo Maafisa Wakuu Waandamizi wa Makao Makuu ya Polisi ambapo aliwataka maafisa hao kuyatumia vyema mafunzo waliyoyapata ikiwemo eneo la mawasiliano ya kimkakati na uongozi yaliyofanyika jijini Dodoma kwa muda wa siku tano.

Naye Msemaji wa IPRT Bwana William Kalaghe amesema kuwa, taasisi yake itaendelea kutoa mafunzo kwa Jeshi la Polisi kwa kubadilisha taswira ya Jeshi hilo.

Hata hivyo, bwana Kalaghe ameahidi kutoa kozi maalum kwa Waandishi wa Habari wa Tanzania ili kuweza kulielewa Jeshi la Polisi na kazi wanazozifanya.

Aidha, washiriki wa warsha hiyo walipatiwa vyeti maalum vya ushiriki.

Post a Comment

0 Comments