Ticker

6/recent/ticker-posts

WAFUGAJI WA KUKU 50 WILAYA ZA HANDENI NA MKINGA WAPATIWA MAFUNZO NA KUWEZESHWA VIFARANGA.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Siriel Mchembe akikata utepe ishara ya kuzindua mwongozo wa Taifa wa ufungaji kuku.
Mchembe akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi Shirika la Save the Children Sofia Molamari.
Mratibu wa Uhakika wa chakula Shirika la Save the Children Mkoa wa Tanga Anania Yusto akiongea na washiriki wa Kikako kutoka Wilaya za Handeni na Mkinga.
Kaimu Mkurugenzi Shirika la Save the Children Sofia Molamari akiongea na washiriki.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Siriel Mchembe akiongea na washiriki.


***************************


Na Hamida Kamchalla, TANGA.

WANANCHI wapatao 50 katika Wilaya za Mkinga na Handeni mkoani Tanga wamepatiwa mafunzo ya ufugaji bora wa kuku ikiwa ni pamoja na kukabidhiwa vifaranga 2500 kwa ajili ya kuanza ufugaji.

Msaada huo ambao umegarimu zaidi ya sh milioni 26 umetolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la Save the Children ambao uliambatanishwa na madawa pamoja na vyakula vya kuku lakini pia walipatiwa muongozo wa ufugaji.

Akizindua muongozo huo, mkuu wa Wilaya ya Handeni Siriel Mchembe, kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba amesema mafunzo hayo yametolewa kwa wafugaji 26 kwa Wilaya ya Mkinga na 24 kwa wilaya ya Handeni.

“Na elimu hii inapaswa kusambazwa kwenye jamii zao kwa wananchi wote katika maeneo yao, leo hii wafugaji wote 50 ambao wamepata elimu kila mmoja vifaranga 50, chakula cha kuku cha kuanzia kg 100 ambacho kitatumika kwa muda wa mwezi mmoja pamoja na kunawakabidhi muongozo wa Taifa wa ufugaji”

Aidha Mchembe ametoa shukurani zake kwa Shirika hilo kwa kushirikiana na Shirika la World Vission nchini kwa kuiunga mkono serikali kupitia misaada yao wanayowapatia wananchi na kuigusa moja kwa moja jamii katika maeneo yao.

Amebainisha kwamba mbali na msaada huo tayari mashirika hayo yapo kwenye mpango wa ugawaji wa chakula katika shule za Wilaya hizo ambao unafanya kazi ndani ya miezi mitatu ambao umegarimu zaidi ya sh milioni 500.

Mchembe alisema, "tutahakikisha tunapita katika kila shule ambayo imepatiwa msaada hu kuangalia ule mkeka wa ugawaji wa chakula kule shuleni ndivyo ulivyovika au laa" amesema.

"Lakini pia kuwapitia wazazi waliopokea vyakula hivi, ili kuhakikisha kwamba chakula kilichotolewa na mashirika haya kinawafikia watoto na siyo wajanja wachache kwa maslahi yao na kuwatesa watoto" amesistiza.


Amesema uhakiki huo utakwenda sambamba na kuangalia uhakiki waliojiwekea walimu wa kuhakikisha shule hizo zinaendelea kupata chakula baada ya ile miezi mitatu.

"Lakini vilevile na shule zetu zote katika halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Handeni mji na Handeni Wilaya kuhakikisha suala hili la njaa haliwagusi watoto wetu, niwaombe sana jambo hili mlizingatie" ameeleza.


"Niwaombe sana wakurugenzi na wakuu wa Wilaya mlisimamie jambo hili kwa moyo wenu wote, mkivishirikisha vyombo vyenu vya ulinzi na usalama kuhakikisha kwamba tatizo la njaa haliwatesi wanafunzi wa shule zetu zote" amesisitiza.

Post a Comment

0 Comments