Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS MSTAAFU ALHAJ DKT. KIKWETE ATEMBELEA OFISI NA UKUMBI WA MIKUTANO WA MSIKITI MKUU WA BAKWATA WA MOHAMED WA SITA

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Alhaj Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea sehemu mbalimbali za ofisi na ukumbi wa jengo hilo baada ya kuhudhuri Swala ya Ijumaa katika Msikiti Mkuu wa BAKWATA wa Mohamed wa Sita Kinondoni Muslim jijini Dar es salaam.
Mbunge wa Mchinga Hajjat Salma Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na baadhi ya waumini wenzie baada ya kuhudhuria Swala ya Ijumaa katika Msikiti Mkuu wa BAKWATA wa Mohamed wa Sita Kinondoni Muslim jijini Dar es salaam.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Alhaj Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na viongozi waandamizi wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) baada ya kuhudhuria Swala ya Ijumaa katika Msikiti Mkuu wa BAKWATA wa Mohamed wa Sita Kinondoni Muslim jijini Dar es salaam.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Alhaj Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa katika maktaba katika jengo la ukumbi mpya wa mikutano wa Msikiti Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) wa Mohamed wa Sita Kinondoni Muslim jijini Dar es salaam baada ya kuhudhuria Swala ya Ijumaa.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Alhaj Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na waumini wenzie wakisikiliza mawaidha baada ya Swala ya Ijumaa katika Msikiti Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) wa Mohamed wa Sita Kinondoni Muslim jijini Dar es salaam.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Alhaj Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mbunge wa Mchinga Hajjat Salma Kikwete wakipata picha ya kumbukumbu na viongozi waandamizi wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) baada ya kuhudhuria Swala ya Ijumaa katika Msikiti Mkuu wa BAKWATA wa Mohamed wa Sita Kinondoni Muslim jijini Dar es salaam.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Alhaj Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mbunge wa Mchinga Hajjat Salma Kikwete wakiangalia ukumbi mpya wa mikutano wa Msikiti Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) wa Mohamed wa Sita Kinondoni Muslim jijini Dar es salaam baada ya kuhudhuria Swala ya Ijumaa.


************************


Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Alhaj Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo ametembelea jengo jipya la ofisi pamoja na ukumbi wa mikutano katika Msikiti Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) wa Mohamed wa Sita Kinondoni Muslim jijini Dar es salaam na kufurahishwa na ubora na miundombinu yake ya kisasa.


Alhaj Dkt. Kikwete, aliyeongozana na mkewe Mbunge wa Mchinga Mhe. Hajjat Salma Kikwete, ametembelea jengo hilo mara baada ya kuhudhuria Swala ya Ijumaa katika msikikti huo mkubwa uliojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco.


Akawashauri BAKWATA kuwa wasifanye ajizi katika kuutunza na kuuweka katika mazingira ya usafi msikiti huo na majengo yake ili uendelee kutoa huduma bora kwa waumini katika swala na shughuli mbalimbali za kidini na kijamii kama ulivyokusudiwa.


Akiwa anatembezwa na Katibu Mkuu wa BAKWATA Alhaj Nuhu Jabir Mruma Dkt. Kikwete alitembelea ukumbi wa mikutano wa kisasa pamoja na maktaba ya historia iliyosheheni maandishi ya awali ya Quran Tukufu yaliyoandikwa kwa mikono na wanazuoni wa kale.

Post a Comment

0 Comments