Ticker

6/recent/ticker-posts

SBL KUGAWA MBOLEA BURE KWA WAKULIMA SONGWE

Kaimu Meneja wa Kampuni ya Mbolea Tanzania Kanjel Mloba akimpongea Mkurugenzi wa Kampuni ya Utengezaji Mbolea ya SBL kutoka Kenya Joe Kariuki katika maonyesho hayo

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Waziri Kindamba (kulia) akipata maelezo kuhudu mbolea kutoka kwa Kaimu Meneja wa Kampuni ya Mbolea Tanzania Kanjel Mloba,aliozindua Maonyesho ya Siku ya Mbolea Duniani inayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Kimondo, Mlowa, Wilayani Mbozi. wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Utengezaji Mbolea ya SBL kutoka Kenya Joe Lariuki Joe akizungumzia na waandishi wa hsbari kuhudu kugawa bure mbolea ya SBL inayozalisha na Kampuni yake kutoka Kenya

************************

NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya utengenezaji na usambazaji wa mbolea kutoka nchini Kenya SBL imetangaza neema kwa wakulima hapa nchini ambapo itatoa mfuko mmoja bure kwa wakulima watakaofika katika Banda lake katika Msonyesho ya Siku ya Mbolea Duniani yanafanyika kitaifa katika Viwanja vya Kimondo,hMlowo,Wilayani Mbozi, mkoani Songwe.

Akizungumzia na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa maonyesho hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Joe Kariuk, amesema watakao nufaika na ofa hiyo ni wakulima watakao fika katika Banda la Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) na kununia mifuko kuanzia mitatu ya mbolea ya SBL Kisha kupewa mfuko mmoja bure.

Joe amesema SBL dhamira ni kuunga mkono jitihada za serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kumwinua mkulima wa kitanzania

"SBL imeonyesha ufanisi mkubwa nchini Kenya. Sasa tunataka hata hapa Tanzania wakulima wanufaike nayo na kwa kuanzia tunatoa mfuko mmoja wa kilo 25 bure kwa wateja watakaofika katika maonyesho haya hapa Songwe,"alisemaJoe.

Amesema SBL kupitia TFC r imeingiza mifuko 2500 ya mbolea hiyo ya organic ambayoni rafiki wa mazingira.

"Mifuko hiyo 2500 ilmeingia Songwe na tutauza na kuigawa bure. Wananchi waje katika uwanja wa Kimondo Mlowo na. Wafike katika Banda la TFC" ameongezs Joe.

Awali Kaimu Meneja wa Kampuni ya Mbolea Tanzania TFC Kanjel Mloba alisema mbolea hiyo ya SBL imeingizwa nchini kutokana na ubors wake na ufanisi huko Kenya.

"Pamoja na mbolea nyingine leo katika maonyesho hayaTF. Tumetambulisha mbolea hii ya SBL ambayo no organic. Ni mbolea nzuri na tunahimiza wakulima kuitumia"amesema Kanjel.

Amesema TFC itaendelea kuhakikisha inawasaidia wakulima kuwafikishia mbolea Bora ili kilimo Chao kiwe chenye Tina.

Maonyesho hayo ya Siku tatu yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania TFRS yameanza leo na yanatarajiwa kufungwa na Wazirii wa Kilimo Hussein Bashe Oktoba 13 mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments