Ticker

6/recent/ticker-posts

TBS YATOA ELIMU YA VIWANGO KWA WAJASIRIAMALI NA WAFANYABIASHARA PWANI.


*********************

Elimu hii imetolewa wakati wa wiki ya uwekezaji na Biashara Pwani iliyofanyika kuanzia tarehe 05/10/2022hadi 10/10/2022 katika viwanja ya Stendi ya maili moja -Kibaha Pwani.

Akizungumza wakati wa Maonesho hayo Mkaguzi (TBS) Bw Issa Dadi amesema shirika limetumia maonesho haya kutoa elimu kuhusu majukumu yake ikiwa ni uthibitishaji wa bidhaa na mifumo, usajili na majengo na bidhaa za chakula na vipodozi, upimaji, uandaaji wa viwango na udhibiti wa bidhaa kwa bidhaa zinanotoka nje ya nchi.

“TBS ni shirika lililopewa dhamana ya kusimamia ubora wa bidhaa zinazozalishwa nchini na zile zinatoka nje ya nchi hiyo basi wazalizaji, wasambazaji, waagizaji wa bidhaa nje ya nchi na wafanyabiashara wanatakiwa kuhakikisha bidhaa wazaozalisha na zile zinazotoka nje ya nchi zimethibishwa na kukidhi matakwa ya viwango kabla ya kuingizwa sokoni” alisema Dadi

Aliongeza kuwa wananchi kama watumiaji wa bidhaa wao wananafasi kubwa ya kufanya katika kuhakikisha bidhaa zilipo sokoni zimekidhi matakwa ya Viwango kwani wao ndio wanofanya maamuzi ya kununua au kutokununua bidhaa

“Wananchi kama watumiaji wa mwisho wa bidhaa ndio waathirika wakubwa wa bidhaa hafifu na endapo watajenga utamaduni wa kununua bidhaa zile tu ambazo zimethibitishwa ubora wake taratibu lakini kwa hakika soko la Tanzania litajazwa na bidhaa zilizokidhi matakwa ya viwango tu na kwa pamoja kama Taifa tutakuwa tumeishinda vita ya bidhaa hafifu.

Jukumu la kuhakikisha Tanzania inakuwa na bidhaa zilizokidhi matakwa ya Viwango si la TBS pekee yake bali ni jukumu la kila Mtanzania kuanzia mzalishaji wa bidhaa, muagizaji wa bidhaa nje ya nchi,msambazaji wa bidhaa, muuzaji wa bidhaa na mtumiaji wa bidhaa. Hiyo basi tukiamua kwa pamoja tutajenga Taifa salama na kukuza uchumi wa nchi kwani bidhaa zetu zitakubalika katika masoko ya kitaifa na kimataifa. Alisisitiza Bw. Dadi

Post a Comment

0 Comments