Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Prof. Tumaini Nagu (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Health Promotion Support (THPS), Dkt. Redempta Mbatia (kulia), na Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya THPS, Dkt. Rumishael Shoo, wakionesha vitabu vya Mpango Mkakati wa Tatu wa THPS wa miaka mitano (2026–2030), jijini Dar es Salaam. 
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Prof. Tumaini Nagu, akizindua rasmi Mpango Mkakati wa Tatu wa Tanzania Health Promotion Support (THPS) wa miaka mitano (2026–2030), jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Prof. Tumaini Nagu, akizindua rasmi Mpango Mkakati wa Tatu wa Tanzania Health Promotion Support (THPS) wa miaka mitano (2026–2030), jijini Dar es Salaam.
Viongozi na washiriki mbalimbali wakipiga makofi wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Tatu wa Tanzania Health Promotion Support (THPS) wa miaka mitano (2026–2030), jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Prof. Tumaini Nagu, akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Health Promotion Support (THPS), Dkt. Redempta Mbatia (kulia), kitabu kinachoelezea Mpango Mkakati wa Tatu wa THPS wa miaka mitano (2026–2030), jijini Dar es Salaam.
Viongozi wakionesha vitabu vya Mpango Mkakati wa Tatu wa Tanzania Health Promotion Support (THPS) wa miaka mitano (2026–2030), jijini Dar es Salaam.
Viongozi wakionesha vitabu vya Mpango Mkakati wa Tatu wa Tanzania Health Promotion Support (THPS) wa miaka mitano (2026–2030), jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Prof. Tumaini Nagu, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Tatu wa Tanzania Health Promotion Support (THPS) wa miaka mitano (2026–2030), jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Prof. Tumaini Nagu, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Tatu wa Tanzania Health Promotion Support (THPS) wa miaka mitano (2026–2030), jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Prof. Tumaini Nagu, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Tatu wa Tanzania Health Promotion Support (THPS) wa miaka mitano (2026–2030), jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Health Promotion Support (THPS), Dkt. Redempta Mbatia, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Tatu wa THPS wa miaka mitano (2026–2030), jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Health Promotion Support (THPS), Dkt. Redempta Mbatia, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Tatu wa THPS wa miaka mitano (2026–2030), jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Health Promotion Support (THPS), Dkt. Redempta Mbatia, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Tatu wa THPS wa miaka mitano (2026–2030), jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS), Dkt. Rumishael Shoo, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Tatu wa THPS wa miaka mitano (2026–2030), jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Tanzania Health Promotion Support (THPS), Bw. George Anatory, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Tatu wa THPS wa miaka mitano (2026–2030), jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Health Promotion Support (THPS), Dkt. Redempta Mbatia, akimwelezea Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Prof. Tumaini Nagu, kuhusu mikakati ya THPS hadi kufikia Mpango Mkakati wa Tatu (2026–2030), jijini Dar es Salaam.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) limezindua Mpango Mkakati wake wa Tatu (2026–2030), unaoweka mwelekeo wa miaka mitano wa kukabiliana na vipaumbele vya afya nchini Tanzania, huku ukiimarisha mifumo ya afya na jamii, matumizi yenye uwajibikaji ya ubunifu wa kidijitali na teknolojia, pamoja na kupanua vyanzo vya fedha na ushirikiano kwa ajili ya ufadhili endelevu wa huduma za afya.
Mpango huo umezinduliwa rasmi Septemba 23,2026 jijini Dar es Salaam na Prof. Tumaini Nagu, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
Hafla hiyo imewakutanisha viongozi waandamizi kutoka Serikali na Mamlaka za Serikali za Mitaa, washirika wa maendeleo, asasi za kiraia, taasisi za elimu ya juu na utafiti, sekta binafsi, taasisi za uhisani, waanzilishi na wanachama wa THPS, Bodi ya Uongozi, wafanyakazi pamoja na vyombo vya habari.
Mpango Mkakati umeandaliwa kwa kuzingatia vipaumbele vya afya vya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mafanikio yaliyopatikana kupitia Mpango Mkakati wa 2021–2025. Unazingatia pia mabadiliko ya mazingira ya afya ya umma, yakiwemo mabadiliko ya mifumo ya magonjwa, vitisho vipya vya kiafya, athari za mabadiliko ya tabianchi, maendeleo ya teknolojia na mabadiliko katika ufadhili wa afya duniani.
Akizindua Mpango Mkakati huo, Prof. Nagu ameipongeza THPS kwa kuweka ushirikiano, ustahimilivu wa mifumo, uendelevu na ubunifu kuwa sehemu muhimu ya mwelekeo wake wa baadaye.
Amesisitiza umuhimu wa programu za washirika kuendana na vipaumbele vya Serikali na kuimarisha mifumo iliyopo badala ya kuanzisha mifumo sambamba.
“Changamoto za afya zilizo mbele yetu zinahitaji ushirikiano imara na suluhisho endelevu. Tunakaribisha washirika wanaoelekeza uwekezaji wao katika vipaumbele vya kitaifa, wanaoimarisha mifumo yetu ya afya na kusaidia kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi popote wanapoishi. Mpango Mkakati huu unaweka msingi muhimu kwa THPS kuendelea kuchangia katika ajenda hii ya pamoja ya kitaifa,” amesema Prof. Nagu.
Prof. Nagu pia amesisitiza umuhimu wa huduma za afya ya msingi, huduma na bima ya afya kwa wote, uhamasishaji wa rasilimali za ndani, uzalishaji wa bidhaa za afya nchini, mageuzi ya kidijitali na maamuzi yanayozingatia ushahidi.
Amehimiza utekelezaji wa mkakati huo kuleta maboresho yanayopimika katika huduma na matokeo ya afya.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia, amesema mkakati mpya utaendeleza mafanikio yaliyopatikana huku ukiweka mwelekeo wa kukabiliana na changamoto za afya zinazoibuka.
“Mpango Mkakati huu unakuja katika kipindi muhimu kwa Tanzania na jumuiya ya afya duniani. Mahitaji ya afya yanabadilika, teknolojia inabadilisha namna huduma zinavyoweza kutolewa, na mazingira ya ufadhili pia yanabadilika. Hivyo, tunapaswa kuendana na mabadiliko hayo huku tukiendelea kuweka mbele maslahi ya watu na jamii tunazozihudumia,” amesema Dkt. Mbatia.
Amebainisha kuwa THPS inaingia katika kipindi hiki ikiwa na msingi imara uliojengwa kupitia ushirikiano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jamii, asasi za kiraia, sekta binafsi na washirika wa maendeleo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya THPS, Dkt. Rumishael Shoo, ameelezea uzinduzi huo kuwa hatua muhimu katika dhamira endelevu ya THPS ya kuboresha afya na ustawi wa Watanzania. Alisema mkakati huo unajengwa juu ya uzoefu wa THPS huku ukiliweka shirika katika nafasi ya kukabiliana na changamoto na fursa zinazoibuka.
“Wajibu wetu si tu kuweka mwelekeo wenye malengo makubwa kwa THPS, bali pia kuhakikisha mkakati huu unatekelezwa kwa uongozi imara, uwajibikaji na msisitizo wa wazi katika matokeo yatakayoboresha afya na ustawi wa Watanzania,” amesema Dkt. Shoo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa THPS, Bw. George Anatory, amesema uandaaji wa Mpango Mkakati wa Tatu umechangiwa na mtandao mpana wa washirika, wakiwemo Serikali, washirika wa maendeleo, taasisi za elimu na utafiti, asasi za kiraia na jamii, sekta binafsi, pamoja na Bodi ya Uongozi, Menejimenti na wafanyakazi wa THPS.
“Tunasonga mbele pamoja, tukipima mafanikio si kwa idadi ya taarifa tunazotoa tu, bali kwa maisha yenye afya bora zaidi nchini Tanzania na kwingineko,” amesema Bw. Anatory.
Katika kipindi cha mpango mkakati uliopita, THPS ilichangia katika afua za VVU na kifua kikuu; afya ya uzazi, mama, mtoto mchanga na kijana; magonjwa yasiyoambukiza; afya ya akili; na kukabiliana na vitisho vinavyoibuka vya afya ya umma. Shirika pia lilichangia kuimarisha mifumo ya taarifa za afya, ugavi na mifumo ya kijamii katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mpango Mkakati wa Tatu wa THPS (2026–2030) unabainisha maeneo kumi ya matokeo muhimu yatakayoongoza utekelezaji wa programu na maendeleo ya taasisi katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Maeneo hayo ni afya ya uzazi, mama, mtoto na kijana; usalama wa afya duniani na magonjwa yanayoibuka; magonjwa ya kuambukiza na magonjwa ya kitropiki; magonjwa yasiyoambukiza na afya ya akili; uhamasishaji wa afya, mawasiliano kuhusu vihatarishi na ushirikishwaji wa jamii; ulinzi wa ustawi wa jamii na msaada wa kisaikolojia; mabadiliko ya tabianchi, mazingira na afya; ufadhili endelevu na usimamizi wa vihatarishi; ubunifu wa kidijitali, akili unde (AI) na uimarishaji wa mifumo; pamoja na utawala wa kitaasisi na uwezo wa shirika.
Mkakati unaweka msisitizo katika ubunifu wa kidijitali na matumizi yenye uwajibikaji ya akili unde (AI), ikiwemo katika ufuatiliaji wa magonjwa, maamuzi ya kitabibu na kiprogramu, usimamizi wa maabara na mifumo ya ugavi, mwendelezo wa huduma na upatikanaji wa huduma za afya. Matumizi hayo yatazingatia sera na viwango vya Serikali, usalama wa kimtandao, ulinzi wa taarifa, maadili na usimamizi wa binadamu.
Kutokana na mabadiliko katika mazingira ya ufadhili wa afya duniani, mkakati unaweka pia msisitizo katika uendelevu wa kifedha na upanuzi wa ushirikiano. THPS itaendelea kushirikiana na washirika wa maendeleo huku ikipanua ushirikiano na Serikali, sekta binafsi, wawekezaji wa ndani, taasisi za uhisani na wadau wengine, ikiwemo kupitia ubia kati ya sekta ya umma na binafsi na fursa nyingine za uhamasishaji wa rasilimali za ndani.
Mpango Mkakati wa Tatu utaongoza programu za THPS katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa lengo la kusaidia utoaji wa huduma jumuishi za afya na ustawi wa jamii kupitia uhamasishaji wa afya, kinga, huduma, matibabu na utafiti, kwa kushirikiana na Wizara za Afya Tanzania Bara na Zanzibar, wizara nyingine husika na wadau katika ngazi za kitaifa, mikoa, wilaya na jamii.
Dira ya mkakati huu ni “Jamii ya Watanzania yenye afya ambapo kila mtu ana fursa sawa ya kupata huduma za afya zenye ubora wa hali ya juu.”
Tanzania Health Promotion Support (THPS) ni shirika la kitaifa lisilo la kiserikali, linaloshirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na washirika wengine katika kuhamasisha na kusaidia upatikanaji wa huduma za afya zenye usawa, ubora wa hali ya juu, zinazofikika na endelevu.
Kupitia programu zake, tafiti, uimarishaji wa mifumo ya afya na jamii pamoja na ushirikiano wa kimkakati, THPS inachangia juhudi za kitaifa za kuboresha afya na ustawi wa Watanzania.
0 Comments