Ticker

6/recent/ticker-posts

UDSM YATOA HAMASA KWA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU


********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KATIKA Kuadhimisha Miaka 60 ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, leo Oktoba 19,2022 Shule Kuu ya Elimu imetembelea shule mbalimbali ikiwemo shule ya Sekondari Jangwani pamoja na Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa kuwapa hamasa wanafunzi wenye ulemavu ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Amidi, Shule Kuu ya Elimu Dkt.Eugenia Kafanabo amesema katika kusheherekea maadhimisho hayo wameamua kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu katika shule za sekondari zilizopo Jijini Dar es Salaam.

Chuo kiliongozana na watu wenye ulemavu ambao wamepambana na kufanikiwa ikiwa ni njia moja wapo ya kuwafanya wanafunzi wenye ulemavu wasikate tamaa kwenye masomo yao waongeze bidii ili waweze kufanikiwa.

Aidha Dkt.Kafanabo amewataka wanafunzi wenye ulemavu kutokujiona hawafai kwenye jamii bali wajione wanaweza hivyo kupita Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitaendelea kushirikiana na shule ambazo kuna wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Post a Comment

0 Comments