Ticker

6/recent/ticker-posts

PRECISION AIR YATANGAZA KUONGEZA SAFARI ZA NDEGE KUTOKA TANZANIA KWENDA NCHINI COMOROS.**********************

Emmanuel kawau.

Kufuatia wito uliotolewa na balozi wa Comoros nchini wa fursa za kibiashara zilizopo nchini humo hii leo Shirika la Ndege la Precision Air nchini limetangaza kuongeza idadi ya safari zake za ndege kutoka Tanzania kwenda nchini Comoros hadi mara tatu kwa wiki.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam Balozi wa Comoros nchini Tanzania Dkt. El Badaoui Fakih amesema ongezeko la safari za ndege umekuja wakati ambao mahitaji ya usafiri wa anga kati ya Tanzania na comoros umekuwa mkubwa zaidi.

Aidha amesema kurejea kwa safari hizo ambazo zilisitishwa mwaka 2012 kutaendelea kukuza ushirikiano baina ya Tanzania na Comoro kwani wananchi wengi wa Comoro wanaishi nchini Tanzania toka zamani ambapo kuna maeneo mbalimbali yanayodhibitisha hilo ikiwemo Msikiti wa Ngazija hivyo Tanzania na Comoro ni ndugu.

Ameongeza kuwa pamoja na Precision Air kuiunganisha Tanzania na Visiwa vya Comoro pia wameiunganisha Moroni(Hahaya) na Anjouan jambo ambalo limeimarisha huduma za usafiri wa anga nani ya visiwa hivyo ambapo amewaomba watanzania kufanya safari za kutembelea Comoro.

“Tulipowajulisha Precision Air uwepo wa fursa katika sekta ya usafiri wa anga haikuwachukua muda kuchangamkia fursa hiyo na tulishuhudia weledi wa hali ya juu kutoka kwao hivyo kwaniaba ya serikali ya comoros inayoongozwa na Mh. Rais Azali Assoumani tunapenda kuwapongeza na kuwashukuru Precision Air kwa huduma zao za uhakika" amesema Balozi Fakhi.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa Precision Air Bw. Patrick Mwanri ameishukuru serikali ya comoros kwa fursa iliyotolewa na shirika la ndege la precision Air kuendesha safari za ndege za ndani na nje na kumuhakikishia kuwa wapo tayari kutoa huduma za haraka ,uhakika na nafuu.

"Katika uchumi wa Dunia ya sasa huduma za usafiri wa anga ni kichocheo muhumi cha ukuaji wa uchumi na tumejiandaa kusaidia uhusiano na ukuaji wa kiuchumi.tulirejesha safari zetu kuanzia tarehe 13/7/2022 ikiwa ni kuitikis wito kutoka serikali ya comoros. Mapokezi ya huduma zetu yamekuwa mazuri na leo takribani miezi mitatu tunafurahi kutanganza ongezeko la safari mbili hadi tatu kwa wiki" Alisema Mwanri.

Aidha kutokana na muitikio kuwa mzuri wa serikali ya comoros precision Air itaanza mikakati ya kuongeza safari za ndege na kuwa za kila siku.

Post a Comment

0 Comments