Ticker

6/recent/ticker-posts

WAKILI DKT.LUHENDE AMUHAKIKISHIA USHIRIKIANO NAIBU WAKILI MKUU WA SERIKALI BI.MWAIPOPO

Wakili Mkuu wa Serikali Dkt.Boniface luhende (kulia) akimkabidhi nyaraka za ofisi ya Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi.Sarah Mwaipopo ambaye ni Naibu Wakili Mkuu wa Serikali katika hafla ya kuwapongeza kwa kuteuliwa na Rais Samia Suluhu kushika nyadhfa hizo. Hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 24,2022 kwenye ofisi za Wakili Mkuu wa Serikali Jijini Dar es Salaam.Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi.Sarah Mwaipopo akiwasili na kupokelewa na wajumbe wa Menejimenti ya ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali leo Oktoba 24,2022 katika Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Jijini Dar es Salaam baada ya kuaaminiwa,kuteuliwa na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan. Wakili Mkuu wa Serikali Dkt.Boniface luhende akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla ya kumpongeza baada ya kuteuliwa na Rais Samia Suluhu kushika nyadhfa hiyo. Hafla hiyo ambayo imefanyika leo Oktoba 24,2022 ilienda sambamba na kumkaribisha Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi.Sarah Mwaipopo ambaye nae ameteuli hivi karibuni. Wakili Mkuu wa Serikali Dkt.Boniface luhende akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kumpongeza baada ya kuteuliwa na Rais Samia Suluhu kushika nyadhfa hiyo. Hafla hiyo ambayo imefanyika leo Oktoba 24,2022 ilienda sambamba na kumkaribisha Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi.Sarah Mwaipopo ambaye nae ameteuli hivi karibuni. Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Bw.James Kibamba akizungumza katika hafla ya kuwapongeza Wakili Mkuu wa Serikali Dkt.Boniface luhende na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi.Sarah Mwaipopo kwa kuteuliwa na Rais Samia Suluhu kushika nyadhfa hizo. Hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 24,2022 kwenye ofisi za Wakili Mkuu wa Serikali Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Bw.James Kibamba akizungumza katika hafla ya kuwapongeza Wakili Mkuu wa Serikali Dkt.Boniface luhende na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi.Sarah Mwaipopo kwa kuteuliwa na Rais Samia Suluhu kushika nyadhfa hizo. Hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 24,2022 kwenye ofisi za Wakili Mkuu wa Serikali Jijini Dar es Salaam

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*******************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Wakili Mkuu wa Serikali Dkt.Boniface luhende amesema Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imepiga hatua Kutokana na juhudi za watumishi katika kutekeleza majukumu yao hasa katika kudumisha Haki kwa ustawi wa Serikali.

Wakili Boniface Ameyasema hayo Leo Oktoba 24,2022 Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya Pongezi na kupokelewa na Watumishi wa Ofisi hiyo baada ya kuteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan Kushika Wadhfa huo.

Awali Wakili Boniface alikuwa akifanya kazi katika Ofisi hiyo kama Naibu Wakili Mkuu wa Serikali.

Hata hivyo Wakili Boniface ametoa wito kwa watumishi wa Ofisi hiyo Kushirikiana katika kufanikisha majukumu ya Ofisi hiyo ya kufanya suluhu na kulinda Haki pamoja na kulitumika Taifa.

Kwa upande wake Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi.Sarah Mwaipopo amesema atahakikisha anatoa ushirikiano kwa wajumbe wa menejimenti ili weledi wa kazi uweze kuonekana.

"Watumishi wenzangu ambao mnasaidiana nami kutekeleza majukumu ya ofisi kama yalivyoelezwa hapa, mtambue kuwa wote tuna wajibu wa kusimamia vema rasilimali watu na fedha kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma ili kuwa na utendaji wenye tija". Amesema

Aidha amempongeza Rais kwa kumuamini, kumteua na kumuapisha kwa nafasi hiyo ambayo amepatiwa hivyo atahakikisha analeta matokeo makubwa na ufanisi kwa lengo la kuendelea kujenga taswira nzuri iliyopo kwa wadau wao, wananchi na Taifa kwa ujumla.

Hata hivyo amempongeza Wakili Mkuu wa Serikali Dkt.Boniface Luhende pamoja na wajumbe wa menejimenti ya ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa mapokezi makubwa ambayo wameyafanya kwake.

Post a Comment

0 Comments