Ticker

6/recent/ticker-posts

BODI PSSSF YAKAGUA UKARABATI KIWANDA CHA CHAI MPONDE

*Ukarabati umekamilika, kinazalisha

*Kitasaidia zaidi ya wakulima 3500

Na Mwandishi Wetu, Lushoto

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mhandisi Musa Iyombe amerBODI PSSSF YAKAGUA UKARABATI KIWANDA CHA CHAI MPONDEidhishwa na ukarabati uliofanyika katika kiwanda cha Chai cha Mponde. Sasa kiwanda hicho kimenza uzalishaji.

Mhandisi Iyombe alisema hayo mwishoni mwa wiki, ambapo yeye, akiongozana na wajumbe wengine wa Bodi ya Wadhamini wa PSSSF walitembelea kiwanda hicho kilichopo katika kijiji cha Kweminyasa,wilayani Lushoto ili kukagua maendeleo ya ukarabati wa kiwanda hicho.

“Tumetembelea kiwanda hiki cha Mponde ambacho kinazalisha chai bora, chai nzuri ambayo inaweza ikatumika ndani na nje ya nchi. Kiwanda kipo vizuri baada ya ukarabati, tumeona kiwanda kimeanza kuchakata majani ya chai, naamini wakulima wenye mashamba kwenye wilaya ya Lushoto, hususan Bumbuli, Korogwe na maeneo jirani watanufaika sana na uwepo wa kiwanda hiki” alisema Mwenyekiti wa Bodi ya PSSSF.

Mhandisi Iyombe alisema kuanza uzalishaji kwa kiwanda cha Chai Mponde ni wazi kwamba vijana wengi watapata ajira na kwamba uchumi wa kata ya Mponde na wilaya ya Lushoto, ikiwemo Bumbuli na maeneo jrani utakuwa iwapo fursa ya kuwepo kwa kiwanda itatumiwa vyema.

Kwa upande wake, Meneja wa Kiwanda hicho, Bi.Sane Kwilabya alisema, “kwa upande wetu tumejipanga vyema kuzalisha chai bora katika kiwanda hiki, na tunaamini ardhi ya huku ni nzuri kwa kilimo cha majani ya chai yaliyo bora."

Msimamizi wa ukarabati wa mradi huo, Mhandisi Ally Shanjirwa alisema ukarabari wa kiwanda hicho umekamilika kwa asilimia mia moja (100%) na sasa kinachofanyika ni kujaribu mitambo ili kubaini dosari na kuzirekebisha.

Kiwanda cha Chai Mponde kinaendeshwa kwa pamoja kati ya PSSSF na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kupitia kampuni ya Mponde Holding Company Limited, ambapo kila Mfuko umewekeza asilimia 42 na Msajili wa hazina anamiliki hisa 16.

Kiwanda kinategemewa kuzalisha ajira za muda mrefu zisizopungua 79 na ajira za muda mfupi zinazokadiriwa kuwa kati ya 100 hadi 300 kutegemea na msimu wa mavuno ya majani ya chai.

Uwepo wa kiwanda cha Chai Mponde kitaongeza kipato kwa wakulima wa chai katika Halmashauri ya Bumbuli na maeneo jirani, kuongeza mapato kwa taifa kupitia kodi mbalimbali na kuongeza kipato cha fedha za kigeni kwa taifa kupita mauzo ya nje ya chai ya Mponde.

Meneja wa Kiwanda cha Chai Mponde, Bi. Sane Kwilabya (kulia) akitoa maelezo juu ya uzalishaji wa chai kwa wajumbe wa Bodi ya PSSSF wakiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Musa Iyombe (kushoto)

Mwenyeki wa Bodi ya PSSSF, Mha. Musa Iyombe (kulia) akipata maelezo juu ya aina mbalimbali za chai zinazozalishwa katika kiwanda cha Mponde kutoka kwa Menaja wa Kiwanda hicho, Bi.Sane Kwilabya.

Wajumbe wa Bodi ya PSSSF wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya kiwanda cha Chai cha Mponde kilichokarabatiwa.

Post a Comment

0 Comments