Ticker

6/recent/ticker-posts

ZAIDI YA WANANCHI MILIONI 1.6 MKOANI MWANZA WAPATIWA CHANJO YA UVIKO 19

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Thomas Rutachunzibwa akizungumza kwenye kikao cha majadiliano ya tathimini ya chanjo ya uviko 19 na uhuru wa mwendelezo wa kuripoti taarifa za chanjo kilichohusisha waandishi wa habari 30 kutoka vyombo mbalimbali.
Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoani Mwanza (MPC) Edwin Soko akizungumza na waandishi wa habari kwenye kikao cha majadiliano ya tathimini ya chanjo ya uviko 19 na uhuru wa mwendelezo wa kuripoti taarifa za chanjo kilichohusisha waandishi wa habari 30 kutoka vyombo mbalimbali.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Thomas Rutachunzibwa kwenye kikao cha majadiliano ya ya tathimini ya chanjo ya uviko 19 na uhuru wa mwendelezo wa kuripoti taarifa hizo yaliyolatibiwa na klabu wa Waandishi wa Habari mkoani Mwanza (MPC) na kufadhiliwa na shirika la Internews kupitia mradi wa Boresha Habari.


*******************

Na Sheila Katikula,Mwanza

Zaidi ya wananchi milion 1.6 mkoani Mwanza wamepewa chanjo ya uviko 19 na kupelekea idadi hiyo kukamilisha lengo la kitaifa kwa kutoa chanjo hiyo kwa asilimia 87.

Hayo yamesemwa jana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Thomas Rutachunzibwa wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye kikao cha majadiliano ya tathimini ya chanjo ya uviko 19 na uhuru wa mwendelezo wa kuripoti taarifa hizo.

Amesema idadi hiyo ni kwa watu waliokamilisha dozi zote kila mtu anawajibu wa kuelimisha jamii ili kuweza kuwafikia watu wote ambao hawajapata chanjo hiyo.

Amesema lengo la kitaifa ni asilimia 75 ya watanzania kupewa chanjo lakini Mkoa umevuka lengo Kwa kutoa kwa asilimia 87.

"Tunayo kazi kubwa ya kuhakikisha watu waliobaki 200000 wanapata chanjo hiyo ili kuilinda jamii kupata ugonjwa wa corona.

“Kuna uwezekano idadi ya watu inazidi tuliyoilenga lakini tunaendelea na utoaji wa chanjo ili kuhakikisha kila mtu anapachanjwa," amesema Dk Rutachunzibwa.

Hata hivyo amesema zoezi hilo lilianza agosti mwaka jana kulikuwa na upotosha jamii na kupelekea kusambaa kwa taarifa za taharuki zisizothibitishwa na watalaam.

"Zoezi hili lilianza mwaka jana tulianza na makundi ya wazee wenye umri wa miaka 50 na kuendelea, watu wenye magonjwa sugu, wataalamu wa afya,uhamiaji kwa sababu wanakutana watu wengi ni rahisi kuambukizwa ugonjwa huo.

Hata hivyo amewataka waandishi wa habari kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kupatiwa chanjo ya Uviko-19.

Rutachunzibwa amewataka wananchi kuendelea kuzingatia kanuni na taratibu za kujikinga ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara, kuepuka misongamano isiyo ya lazima, kutumia vitakasa mikono mikono na kula chakula bora kwa ajili ya kuimarisha kinga ya mwili ili kuuwezesha kupambana na magonjwa ikiwemo Uviko-19.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Mwanza (MPC), Edwin Soko amesema majadiliano hayo yamelatibiwa na MPC na kufadhiliwa na shirika la Internews kutipia mradi wa 'Boresha Habari' wenye lengo la kuandika habari na kuhamasisha jamii waweze kupata chanjo hiyo sanjari na kutoa elimu kwa waandishi wa habari kuzingatia weledi wanapoandaa maudhui kabla ya kuyafikisha kwa wananchi.

Aidha Mratibu wa Elimu ya Afya kutoka ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akiwasilisha mada kwenye majadiliano hayo yaliyohusisha waandishi wa habari 30 wa mkoani hapa, Renard Mlyakado, amesema lengo la kitaifa Mkoa umefikia asilimia 87 ya uchanji chanjo hiyo kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea.

Mlyakado amesema halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe ikishika nafasi ya kwanza kwa kuchanja kimkoa ambapo asilimia 98.4 wamechanja chanjo hiyo huku ilioshika nafasi ya mwisho ni Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ambayo Ina asilimia 74.3.

“Mafanikio ya kuchanja idadi hiyo ni kutumia vyombo vya habari ikiwemo kutengeneza vipindi maalum vya kuhamasisha utoaji wa chanjo,ushirikishwaji wa viongozi wa serikali za mtaa,ambapo kwa pamoja kumesaidia wananchi kujitokeza kwenda kuchanja huku waliojitokeza zaidi ni wanawake wakiwemo wajawazito,”amesema Mlyakado.

Mlyakado, ameeleza kuwa kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), tangu kutokea kwa mlipuko wa uviko-19 duniani kwa Tanzania jumla ya visa 39, 679 vya uviko-19 vimeripotiwa huku vifo vikiwa 845.

Huku kwa idadi ya kidunia zaidi ya watu milioni 621.7 wameripotiwa kupata virusi na zaidi ya watu milioni 6.5 wakiripotiwa kufariki.

Aidha amesema kuwa kwa mujibu wa WHO katika kipindi hicho hadi sasa zaidi ya chanjo milioni 12.7,zimeshatolewa na kwa kipindi cha masaa 24 yaliyopita visa vipya 164, 921 vya maambukizi ya uviko-19 vimeripotiwa huku vifo vipya 274 vimetokea.

Post a Comment

0 Comments