Ticker

6/recent/ticker-posts

DC BULEMBO AWAONYA WENYE TABIA YA KUFANYA SHUGHULI ZA UCHIMBAJI WA MADINI KWENYE VYANZO VYA MAJI

MKUU wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo akizungumza wakati wa ziara ya wadau kutembelea chanzo cha maji cha mto Zigi iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa mradi wa majaribio wa utunzaji wa vyanzo vya maji kijiji cha Kwemwewe kata ya Mbomole Tarafa ya Amani wilayani Muheza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Ghalib RIngo.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Mazingira y Asili ya Amani Fikiri Maiba akizungumza wakati wa ziara hiyo
MKUU wa wilaya ya Pangani Ghalib Ringo akizungumza wakati wa ziara hito

Afisa Mradi wa Mfuko wa Uhifadhi wa Milima ya Tao la Mashariki Magreth Victor akizungumza wakati wa ziara hiyo.


Na Oscar Assenga, MUHEZA

MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Halima Bulembo amewaonya wananchi wenye tabia za kuvamia vyanzo vya maji na kuchimba madini Tarafa ya Amani wilayani Muheza kuacha mara moja vitendo hivyo kabla hawaja kumbana na mkono wa sheria.


Bulembo aliyasema hayo wakati wa ziara ya wadau kutembelea chanzo cha maji cha mto Zigi iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa mradi wa majaribio wa utunzaji wa vyanzo vya maji kijiji cha Kwemwewe kata ya Mbomole Tarafa ya Amani wilayani Muheza


Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba wamejipanga vilivyo kuhakikisha wanaohusika na vitendo vya namna hiyo wanashughulikiwa ili kuweza kuvimaliza kwa lengo la kuwezesha vyanzo vya maji vinaendelea kuwa salama.


"Kumekuwa na tabia ya wananchi kuvamia maeneo ya vyanzo vya maji wananchi kufanya shughuli za uchimbaji wa madini jambo ambalo lina sababisha uharibifu kwenye vyanzo hivyo ikiwemo uchafuzi"Alisema Mkuu huyo wa wilaya.


Alisema kutokana na uwepo wa athari hizo kubwa kwa jamii watahakikisha wanakula sahani moja na wahusika ili iweze kuwa fundisho kwa wengine ambao wame kuwa na tabia kama
hizo.


" Uchimbaji wa madini ya dhahabu kwenye vyanzo vya maji kuna athari kubwa sana moja hivyo tutawashughulikia wote tutakao wakamata ili kuwezesha vyanzo hivyo vinatunzwa" Alisema.


Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi kuacha kufanya uharibifu kwenye vyanzo vya maji na atayekamatwa na vyombo vya dola sheria itachukua mkondo wake.


"Lakini niwaombe wananchi mtakapowaona walio maeneo ya karibu wafichueni kwa maana vitendo hivyo vina madhara makubwa na kupelekea magonjwa hivyo tunaendelea kuvilinda vyanzo vya maji kwani maji ni uhai" Alisema.


Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo ya wadau Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Mazingira y Asili ya Amani Fikiri Maiba alisema katika eneo hilo kuna chanzo cha maji cha mto Zigi ambacho kinalisha Tanga,Muheza na Mkinga.


Alisema katika vyanzo hivyo kuna uharibifu wa uchimbaji na utafutaji wa dhahabu hivyo jamii inapofuata madini na uharibu huo una madhara makubwa ambacho unapuguzua ubora wa maji kwenye mito.


Alisema katika matumizi hayo kunaleta shida kubwa na hivyo kutumia gharama kubwa kutibu maji hivyo lazima jamii ibadilike kwa ajili ya kulinda vyanzo vya maji.


Hata hivyo alisema kuna hatua mbalimbali zinchukuliwa ikiwemo operesheni na wamepata wahalifu ambao hivi Sasa wanaendelea na kesi hzao hiyo wanatoa wito kuhakikisha vyanzo vya maji ili viweze kuwa endelevu.


Awali akizungumza wakati w ziara hiyo ya wadau Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo alisema kutokana na uharibifu wa vyanzo vya maji wamekuwa wakitumia zaidi ya Bilioni 1 kutibu maji kutokana na uchaguzi ambao umekuwa ukifanyika.


Naye kwa upande wake Afisa Mradi wa Mfuko wa Uhifadhi wa Milima ya Tao la Mashariki Magreth Victor alisema katika kipindi cha nyuma Serikali ilifanikiwa kudhibiti shughuli za uchimbaji wa Madini ya dhahabu kwenye vyanzo vya mto zigi.


Alisema lakini kwa siku za hivi karibuni baadhi ya wananchi wa eneo hilo la Amani wameanza tena shughuli za uchimbaji huo hivyo ipo haja ya hatua za makusudi kuchukuliwa ili kuweza kuendelea kudhibiti vitendo hivyo.

Post a Comment

0 Comments