Ticker

6/recent/ticker-posts

DKT.MPANGO AFUNGUA SHULE YA SEKONDARI UKEREWE ILIYOGHARIMU SHILINGI BILIONI 1.1


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ukerewe mara baada ya kuifungua Rasmi akiwa ziarani Wilayani Ukerewe mkoani Mwanza leo tarehe 25 Novemba 2022.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI David Silinde wakati akikagua majengo ya shule ya Sekondari Ukerewe mara baada ya kuifungua rasmi akiwa ziarani Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza leo tarehe 25 Novemba 2022.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akikagua majengo ya shule ya Sekondari Ukerewe mara baada ya kuifungua rasmi akiwa ziarani Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza leo tarehe 25 Novemba 2022.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya Igala akiwa ziarani Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza leo tarehe 25 Novemba 2022.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akihutubia wananchi wa Wilaya ya Ukerewe katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Getrude Mongela leo tarehe tarehe 25 Novemba 2022.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiagana na wananchi mbalimbali waliojitokeza katika Uwanja wa Getrude Mongela wakati akihitimisha ziara yake wilayani Ukerewe mkoani Mwanza leo tarehe 25 Novemba 2022.

***********************

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 25 Novemba 2022 amefanya ziara ya kikazi ya siku moja katika Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza.

Akiwa ziarani visiwani humo, Makamu wa Rais amefungua rasmi shule ya sekondari ya Ukerewe iliopo kata ya Kagunguri iliogharimu shilingi bilioni 1.1 katika ujenzi wake.

Makamu wa Rais ameiagiza TAMISEMI kuhakikisha shule hiyo inawekewa miundombinu ya somo la fizikia ikiwemo maabara ya somo hilo ili iweze kukamilisha dhana ya sayansi.

Pia Makamu wa Rais ameagiza ujenzi wa shule kuzingatia maendeleo ya sayansi na teknolojia ikiwemo kuweka miundombinu rafiki kwa masomo ya tehama.

Akiwa shuleni hapo Makamu wa Rais amewasihi wazazi na walezi kusimamia Watoto wao wapate elimu ili wawe msaada sahihi kwa maendeleo ya taifa.

Amesema tatizo la mimba za utotoni limekua kubwa wilaya ya Ukerewe na hivyo kurudisha nyuma jitihada za serikali katika kuboresha elimu wilayani hapo.

Makamu wa Rais amesema serikali inaendelea na jitihada za kujenga miundombinu bora ya elimu pamoja kutoa elimu bila malipo kwa elimu ya msingi na sekondari ili kuhakikisha taifa linapata wataalamu wenye tija.

Halikadhalika Makamu wa Rais amekagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya Igala kinachogharimu shilingi milioni 492 katika ujenzi wake.

Ameagiza kituo hicho kukamilika desemba 20 mwaka huu na vifaa tiba kufungwa kabla ya kuisha mwezi februari 2023.

Akiwa katika kituo hicho cha Afya Makamu wa Rais amewasihi watendaji katika maeneo mbalimbali kuchukua kwa umuhimu suala la uhifadhi mazingira ikiwemo kupanda miti na kuifuatilia kwa manufaa ya taifa.

Pia amewataka wananchi kutunza miundombinu ya kituo hicho cha Afya ili kiweze kutoa huduma kwa muda mrefu zaidi.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amezungumza na wananchi wa Wilaya ya Ukerewe katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Getrude Mongela.

Akihutubia katika mkutano huo, Makamu wa Rais amewaasa wananchi wa Ukerewe kujiepusha na vitendo vya uvuvi haramu unaopelekea uharibifu wa mazalia ya samaki na hivyo kuwa na upungufu wa samaki.

Amewataka kufanya jitihada zaidi katika kulinda fukwe zinazozunguka kisiwa hicho pamoja na mazingira kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments