Ticker

6/recent/ticker-posts

DKT.MPANGO MGENI RASMI BAGAMOYO FESTIVAL

Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbasi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuelekea Siku ya Tamasha la 41 la Utamaduni Bagamoyo (Bagamoyo Festival) ambalo linatarajia kufanyika Novemba 10 kwenye Viwanja vya TaSUBa Bagamoyo mkoani Pwani. Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na waandishi wa habari kuelekea Siku ya Tamasha la 41 la Utamaduni Bagamoyo (Bagamoyo Festival) ambalo linatarajia kufanyika Novemba 10 kwenye Viwanja vya TaSUBa Bagamoyo mkoani Pwani. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), Dkt. Herbert Makoye akizungumza na waandishi wa habari kuelekea Siku ya Tamasha la 41 la Utamaduni Bagamoyo (Bagamoyo Festival) ambalo linatarajia kufanyika Novemba 10 kwenye Viwanja vya TaSUBa Bagamoyo mkoani Pwani. Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Zainabu Abdallah akizungumza na waandishi wa habari kuelekea Siku ya Tamasha la 41 la Utamaduni Bagamoyo (Bagamoyo Festival) ambalo linatarajia kufanyika Novemba 10 kwenye Viwanja vya TaSUBa Bagamoyo mkoani Pwani.

*********************

MAKAMU wa Rais, Dkt. Philip Mpango, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la 41 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), linalotarajiwa kuanza Novemba 10, mwaka huu wilayani Bagamoyo.

Dk. Mpango atakuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo msimu huu, kwa kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza na waandishi wa habari Novemba 1,2022 wilayani Bagamoyoi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbasi, amesema walitarajia Rais Samia awe mgeni rasmi lakini atawakilishwa na Makamu wa Rais, Dkt. Mpango.

Amesema wa Dkt. Mpango atakuwa mgeni rasmi na kwamba tamasha litafanyika kwa ukubwa wake ili kuendelea kulipa heshima kwani litashirikisha vikundi kutoka ndani na nje ya nchi.

“Uzinduzi utafanyika Novemba 10, mwaka huu na jioni yake tamasha litaanza rasmi ambapo litashirikisha vikundi vya ndani na nje ya nchi.

“Mgeni rasmi tunatarajia atakuwa Makamu wa Rais Dkt. Mpango ambaye atamwakilisha Rais Samia, kutakuwa na burudani za kila aina na nchi mbalimbali zimeshathibitisha ushiriki wao". Amesema Dkt.Abbasi

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Zainabu Abdallah amesema anawakaribisha wadau mbalimbali wa burudani katika tamasha hilo.

Aidha amesema tamasha la mwaka huu linatarajiwa kuwa tofauti zaidi kwani kutakuwa na tukio la Royal Tour ambapo wadau wa sanaa watatembelea vivutio mbalimbali vya Bagamoyo.

“Tunawakaribisha wadau mbalimbali kujitokeza kwa ajili ya kupata burudani katika tamasha la mwaka huu, maandalizi yamekamilika kwa kiasi kikubwa na tutahakikisha kila mmoja atakayehudhuria ataondoka akiwa ameridhika". Amesema

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), Dkt. Herbert Makoye amesema jumla ya vikundi 27 vya Tanzania vimethibitisha kushiriki huku nane vikitoka nje ya nchi.

Amesema kuwa wameshapata ufadhili kutoka katika maeneo mbalimbali huku wakiendelea kuzungumza na wadau wa sanaa ili kuwaunga mkono.

“Tunaendelea na maandalizi ya tamasha la mwimu huu ambapo litahusisha vikundi 27 kutoka Tanzania na vingine nane kutoka nje ya nchi.

“Kila kitu kinakwenda vizuri kwani tumeshapata ufadhili kutoka kwa watu mbalimbali na tunaendelea kuzungumza na wadau ili watuunge mkono,” Amesema

Post a Comment

0 Comments