Ticker

6/recent/ticker-posts

JUKUMU LA KUOKOTA TAKA NI LA WANANCHI WOTE..


Na Magrethy Katengu

Wananchi wote wameshauriwa kutambua kuwa jukumu la kuwa na kuokota taka kwenye maeneo yanayowazunguka ni wajibu wajibu wao ili kusaidia kuepukana na magonjwa ya mlipuko yatokanayo na uchafu wa mazingira ikiwemo kipindupindu,

Akizungumza Leo na Afisa Tarafa wa Kariakoo Wilaya ya Ilala Mkoani Dar es salaam Christina Kalekezi wakati akizinduzi wa Mpango mkakati wa siku ya waokota taka Duniani iliyofanyika Jijini Dar es salaam ,ambapo Duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo 1 Marchi na Tanzania Maadhimisho yake yatafanyika Machi 9 amesema kuwa bado Jamii inatambua kuwa kazi ya kuokota taka ni ya kikundi maalumu na sio wajibu wa kila Mtanzania.

Hata hivyo Afisa tarafa huyo ambaye akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng'wilabuzi Ludigija kwenye Uzinduzi wa mpango wa siku ya Wakusanya taka Duniani,nakusisitiza kuwa kuwa Jamii ndio inatupa taka hovyo, hivyo inapswa kuendelea kupewa Elimu ya kukusanya nakuzihifadhi sehemu salama.

" Shughuli ya ukusanyaji taka niya serikali lakini nyinyi Wakusanya taka hamlali ,mnaisadia serikali kukusanya taka hizo,kwakweli serikali inatambua mchango wenu wa kuweka mazingira safi" amesema Christina.

Sanjari na hayo alisema taka nyingi zinazozalishwa ni ajira kwani nyingine huenda kuwa mbolea ,taka rejezi pia hufanya mazingira kuwa safi na kuchangia kwa kiasi hivyo ni budi wananchi na kuunga mkono serikali ya awamu ya sita kwa kuweka mazingira safi na salama"

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya "Taka Ni Ajira Foundation" Alen Kimambo amesema siku ya hiyo wataokota nchini Tanzania ikiwa na dhumuni la kutambua kazi ambazo waokota taka wanazifanya katika mazingira magumu na hatarishi nakuwafanya wawe kitu kimoja kwa kupaza sauti zao kwa wadau wa uzalishaji wa taka na serikali kwa ujumla.

"Malengo ya serikali ya kufukia taka ziro hayawezi kufikiwa bila kuwatambua waokota taka ambao wanafanya kazi kwenye maeneo ya mitaani na sehemu zingine,hivyo sisi kama Taka Ni Ajira Foundation na Washirika wetu Nipe Fagio tunajaribu kutengeneza msingi wakiwa na sauti ya pamoja na sio mtu mmoja mmoja" alisema Kimambo.

Nae Mkurugenzi wa Nipe Fagio Anna Rocha amesema kwamba asilimia 60 ya taka zinazopelekwa kurejerezwa zinapitia kwa waokota taka ,hivyo taasisi hii ilianza mwaka 2019 na kampeni yakuwafanya waokota taka ( Waste pickers) watambulike akitolea mfano kikundi cha Wakusanya taka waliopo Bonyokwa kata ya Tabata Segerea Hata hivyo mwenyekiti wa kikundi cha wa waokota taka Bonyokwa John Yusuph, amesema kuwa kipindi akiaza kufanya kazi hiyo alidhalauliwa na Jamii, nakuonekana hafai na hana thamani akikusanya taka huitwa mwizi kwano inapotokea vitu vinaibiwa lawama zinapelekwa kwa Waokota taka,hivyo ameiomba halmashauri ya Ilala iwapatie vitambulisho ili wafanye kazi bila usumbufu. Aidha baadhi ya Waokota taka wameiomba serikali kuwaondolea changamoto zinazowakabili ikiwemo Vifaa vya Kinga ,mikopo ya halmashauri,kutambulika nakupatiwa vitambulisho,huduma ya bima ya afya pamoja na fidia kutoka kwa Makampuni yanayozalisha taka kwani wanapopata tatizo hukosa huduma kwa wakati kutokana changamoto ya kifedha .

Post a Comment

0 Comments