Ticker

6/recent/ticker-posts

JUMLA YA VISIMA 12 KATI YA 197 VYAZIBULIWA KUPUNGUZA KERO YA MAJI JIJINI DAR ES SALAAM


Jumla ya visima 12 kati ya 197 vilivyo agizwa kuzibuliwa kwa ajili ya kutatua changamoto ya Jiji la Dar es Salaam vimefanikiwa kusafishwa na kuingiza lita milioni 3 za maji katika mfumo wa maji wa DAWASA ndani ya siku 4.

Hii imekuja baada ya agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye aliagiza Wizara ya Maji kupitia Mamlaka zake kuvifingua visima hivyo ili kupunguza makali ya mgao wa maji jijini Dr es Salaam.

Akizungumza leo Novemba 5,2022 Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bonde la Mto Wami Ruvu Mhandisi Elibariki Mmasi amesema visima viwili vimefunguliwa jana na leo na kufanya visima vilivyo safishwa kuwa 12 kati ya 197 ikiwa ni katika jitihada za kusaidia kukabiliana na uhitaji wa maji jijini Dar es Salaam ambapo kisima kimoja kilicho safishwa siku ya leo kikiwa eneo la Mwananyamala bado kinauwezo wa kuzalisha lita za maji laki moja kwa saa.

Kwa upande wake Meneja wa Mawasiliano DAWASA Bi.Evalastiing Lyalo amesema baada ya visima hivyo 12 kusafishwa wanategemea mgao wa maji kupungua huku akieleza bado jitihada zinaendelea ili kumalizia visima vilivyo salia kwa haraka ili kukabiliana na changanoto ya maji.

Katika hatua nyengine viongozi wa dini nchini wamewataka watanzania kuendekea kufanya maombi ya kuombea mvua ili kukabilana na ukame ukiopelekea uoungufu wa maji.

Post a Comment

0 Comments