Ticker

6/recent/ticker-posts

KINGMUSIC YAMTAMBULISHA RASMI VANILLAH


*******************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MSANII wa Kizazi kipya Vanillamusic ametambulishwa rasmi kwenye lebo ya King music records ambayo inamilikiwa na msanii Ali Kiba na kuahidi makubwa kwa mashabiki wa musiki nchini na nje ya nchi.

Akizungumza na mwandishi wetu mara baada ya kutambulishwa kwenye lebo msanii huyo ambaye jina lake kamili Fanuel Peter amesema "2022 nilitamka kwa kuamini utakuwa mwaka wenye baraka, Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema hii ya leo kutamka kwamba upendo wake ni mkubwa kwangu, Namshukuru kwa uhai na kipaji ikiwa ni seheme ya kazi na faraja yangu". Amesema

Amesema Muziki wetu hauwezi sogea pasipo kuwepo na upendo hivyo amemshukuru Ali Kiba kuwapa nafasi wasanii wachanga kama yeye na ana imani na uwezo na kipaji chake hivyo atahakikisha anafanya vizuri kwa maendeleo ya kipaji chake pamoja na lebo ambayo inamsimamia

" Nina imani na uwezo na kipaji changu, lakini ili niweze kukamilisha Ndoto yangu Nahitaji support yenu, msanii hajakamilika bila upendo wa mashabiki, furaha yangu itakamilika mkinipokea, kusupport na kufurahia Kazi zangu". Amesema Vanillah.

Post a Comment

0 Comments