Ticker

6/recent/ticker-posts

TAFITI ZABAINI JAMII INAJUA MATATIZO YAKE NA KUYATATUA


TAFITI zimebaini kuwa jamii inajua matatizo yake na inauwezo wa kuyatatua kwa kuungwa mkono na kuwezeshwa katika nyanja mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Kampasi ya DUCE Dkt. Almas Mazigo amesema kwa takribani miaka mitatu wamekuwa wakishiriki katika tafiti zaidi ya Tano zinazohusu maisha ya watu na changamoto wanazokumbana nazo hasa zile zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi.

"Matatizo ya mabadiliko ya tabia nchi msingi wake ni jinsi jamii inavyoelewa na utamaduni waliojijengea,tuliamua ilikuona namna jamii ya wavuvi namna wanavyofikiria juu ya mabadiliko ya tabia nchi na athari zake" Alisema Almasi

Ameongeza kuwa wanajamii wa Kilwa waliwakuta wapo tayari kukabiliana na matatizo wanayokumbana nayo ambapo jamii ya wavuvi wa Kilwa wameweza kupambana na uvuvi haramu kwa kuanzisha mfumo wakusimamia uvuvi wao.

"Tulipofika huko tulishangaa kweli changamoto jamii wanazo na wanazijua kwenye maisha yao lakini watu wamechukua hatua na waliochukua hatua ni watu wa kawaida tu ambao wao ndio wanajua wanvyoathirika kwenye maisha yao ambao wamechukua hatua za kudhibiti uharibifu wa matumbawe kwa kuyaotesha upya,wengine wameamua kupanda mikoko iliyo haribiwa ilikupunguza kasi ya ardhi kuliwa na bahari"

Post a Comment

0 Comments