Ticker

6/recent/ticker-posts

WANANCHI MANYONI WATAKIWA KUWA NA HATI ZA ARDHI ZA KUMILIKI MAENEO YAO

Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa akikabidhi Hati ya kumiliki Ardhi kwa Wananchi wa wilaya hiyo katika hafla iliyoandaliwa na Ofisi ya Ardhi Mkoa wa Singida iliyofanyika juzi. Katikati Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Singida, Shamim Hoza
Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Singida, Shamim Hoza akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mpima Ardhi Mkoa wa Singida Sesaria Martin (katikati) akielekeza jambo wakati wa kukabidhi hatihizo

Zoezi la kukabidhi hati hizo likiendelea.
Hati zikikabidhiwa.


Na Dotto Mwaibale, Manyoni



WANANCHI Wilaya ya Manyoni mkoani Singida wametakiwa kuwa na Hati Milki za maeneo yao ili kupunguza migogoro ya ardhi iliyopo katika wilaya hiyo.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa wakatiwa hafla yakukabidhi hati kwa wananchi waliofanya mchakato wa kupima maeneo yao nakuyalipia hafla iliyofanyika hivi karibuni wilayani humo.

"Migogoro mingi yaa ardhi wilayani hapa inatokana na wananchi wengi kutokuwa na Hati milki za maeneo yao hivyo kuwa changamoto kubwa" alisema Mwagisa..

Alisema kuna haja ya kila mwananchi wa Manyoni kuwa na hati ya kiwanja na shamba ili kuhakikisha migogoro ya ardhi inaisha kabisa au inapungua kwa kiasi kikubwa.

Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Singida, Shamim Hoza alisema mwitikio wa wananchi kumilikisha maeneo yao kwa sasa umekuwa mkubwa kutokana na wananchi wengi kuwa na uelewa mkubwa kuhusu hati miliki.

Hoza alisema wataendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umhimu wa kuwa na hati miliki za maeno yao kwa mkoa mzima wa Singida ili kuhakikisha kila mwananchi anakuwa nayo jambo litakalosaidia kupunguza migogoro ya ardhi.

Alisema pamoja na mwitikio wa wananchi kuwa mkubwa bado kuna changamoto kwa baadhi yao kwa kulalamikia gharama za mchakato mzima unaofanyika kuwamilikisha maeneo yao.

Baadhi ya wananchi wameipongeza ofisi ya ardhi Mkoa wa Singida kwa mchakatohuo na kueleza kuwa upatikanaji wa hati hizo umekuwa rahisi tofauti na awali ambapo walilazimika kwenda Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi jijini Dodoma au Dar es Salaam kwa ajili ya kuzipata.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wamesema changamoto iliyopo kwa sasa ni wananchi wengi kuwa na uelewa mdogo wa wa faida za kuwa na hati milikihizo.



Zoezi la ugawaji hati hizo kwa wananchi wa Wilaya ya Manyoni mkoani hapa linafanyika baada ya wananchi kukamilisha taratibu zote za kisheria za kupatiwa hati hizo.

Post a Comment

0 Comments