Ticker

6/recent/ticker-posts

WATOTO WA IBILISI BADO WAPO, WAZAZI TUSHIRIKIANE KUMALIZA UHALIFU.


*****************

Na Hamida Kamchalla, TANGA.


WANANCHI Mkoa wa Tanga wa wamesisitizwa kuwa na uhiyari wa kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuendelea kutokoneza uhalifu hususani watoto wa ibilisi.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari jijini humo Leo Novemba 14, Kamanda wa pili Mkoa wa Tanga Henry Mwaibambe amesema kazi nzuri ya kupambana na uhalifu wa watoto imefanyika lakini bado hawajakwisha kabisa hivyo kuwaomba wananchi kusaidia kuwafichua.

"Mkoa umefanya kazi nzuri ya kuwadhibiti hawa watoto wa ibilisi, lakini hawakwisha wote, wengine wapo na baadhi yao wanatumia bodaboda kufanya uhalifu, kupora watu wakiwa kwenye usafiri huo" amesema.

Kamanda Mwaibambe amebainisha kwamba bila kuweka mikakati na kuwa na roho ya huruma itakuwa vigumu kuwadhibiti watoto hao kutokana na baadhi ya wazazi kuwakingia kifua watoto wao na kuitetea uhalifu wanaoendeleza iwe kwa wazazi hao kujua au kutokujua.


"Utakuta mtoto amekamatwa kwa uhalifu labda ana bodaboda haina hata namba ya usajili, baada anakuja mzazi wake ofisini analalamika mtoto wake aachiwe kwa kudai hana makosa, anaonewa, hapo hapo anakwambia uchungu wa mwana anajua mzazi,


"Tukitaka hili mzazi utajikuta huu chungu wa mwana unakuwa mkubwa zaidi kwa sababu siku utakuta wananchi wamemuua, sasa nitoe wito kwa wazazi na walezi, tusiwaonee huruma Hawa watoto wetu, wanapofanya uhalifu wanatakiwa kupelekwa sehemu husika ili wakajifunze" amesisitiza.

Kamanda huyo amefafanua kwamba jumla ya pikipiki 20 ambazo nyingine hazina namba za usajili lakini pia magari mawili na vyote vikiwa vimerumika katika matukio ya kihalifu, simu, video, bangi pamoja na pombe haramu ya gongo katika kipindi cha wiki tatu.

Aidha Kamanda Mwaibambe amethibitisha kupatikana kwa silaha 490 katika maeneo mbalimbali ya Wilaya za Mkoa huo ambapo yalikuwemo magobole 457, shotgun 25, raifo 3 na bastola 5 na kusisitiza kwa wale ambao bado wanamiliki silaha kinyume na taratibu wazisalimishe kwa jeshi la polisi.

Post a Comment

0 Comments