Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI UMMY -TANZANIA BADO INA UHABA WA MADAKTARI BINGWA

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango wa kutoa huduma za upasuaji wa kibingwa bila malipo kwa wakazi wa Jiji la Tanga uliofanyika kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo ambao umewezeshwa na Taasisi ya Watumishi Health Check, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Tanga mjini ambap kwa pamoja wamewaleta wataalamu hao wa upasuaji kutoka nchini Uingereza.
WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango wa kutoa huduma za upasuaji wa kibingwa bila malipo kwa wakazi wa Jiji la Tanga uliofanyika kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo ambao umewezeshwa na Taasisi ya Watumishi Health Check, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Tanga mjini ambap kwa pamoja wamewaleta wataalamu hao wa upasuaji kutoka nchini Uingereza.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt Seif Kallage akizungumza wakati wa halfa hiyo



MKUU wa wilaya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Mkurugenzi wa Watumishi Afa Check Dkt Siraji Mtulia akizungumza wakati wa uzinduzi huo
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shilloo akizungumza
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Jonathan Budemu akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Sehemu ya madaktari bingwa wakiwa kwenye uzinduzi




Na Oscar Assenga,TANGA.

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amesema Tanzania bado ina uhaba mkubwa wa Madaktari Bingwa hivyo uwepo wa mpango wa kambi ya upasuaji wa huduma za kibingwa unahitajika sio kwa mkoa wa Tanga bali ni mikoa yote nchini.

Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) aliyasema hayo wakati akizindua mpango wa kutoa huduma za upasuaji wa kibingwa bila malipo kwa wakazi wa Jiji la Tanga uliofanyika kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo.

Alisema hivyo uwepo wa mpango huo utawasaidia wana Tanga na watanzania kwa ujumla kupata matibabu, dawa, vifaa tiba bila gharamu yoyote.

Mpango huo ambao utasaidia kufanya upasuaji utafanywa na madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Peleks Humanitarian Organizationya nchini Uingereza ambapo jumla ya wagonjwa 380 watafaidika kati yao wagonjwa zaidi ya 700 waliofanyiwa uchunguzi.

Kambi hiyo ya matibabu Bingwa ya upasuaji imewezeshwa na Taasisi ya Watumishi Health Check, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Tanga mjini ambap kwa pamoja wamewaleta wataalamu hao wa upasuaji kutoka nchini Uingereza.

Awali akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa Watumishi Afa Check Dkt Siraji Mtulia alisema kuwa upasuaji huo utafanyika kuanzia Novemba 5 hadi 11 mwaka huu na utagharimu milioni 876.

Naye kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt Seif Kallage alisema uwepo wa kambi hiyo ni jitihada za Waziri Ummy kwa sababu ni jukumu ambalo amepewa na Rais Samia Suluhu kuhakikisha afya za watanzania vinaimarika na kuboresha huduma.

Alisema hata ukiangalia ile kampeni ya Mama Samia yeye ndio anaiendeleza amenza na Tanga kwa kushirikiana na Peleck anataendelea na mikoa mengine nchini.

Hata hivyo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Jonathan Budemu alisema kwamba kambi hiyo itaweza kuwasaidia wananchi na katika watu 700 walionwa na madaktari walikuwa hawana uharaka ule na muendelezo wa kambi hii utawasaidia kuweza kuwaonaa.

Alisema katika kambi hiyo watakuwa na changamoto ya vitanda hivyo Mstahiki Meya wale ambao watakosa maeneo ya kuwaweka wanaomba kuwaweka kwenye vituo vyengine baada ya upasuaji kama Ngamiani na Makorora na vya jirani ili wote waweze kupata huduma kwa wakati.

“Lakini pia wasikose huduma kwa sababu ya kukosa sehemu ya kulala kwa sababu vitanda ni vichache ukilinganisha na wagonjwa wenyewe hivyo wakishafanyiwa wakikosa nafasi hapo watapelekwa kwenye maeneo mengine”Alisema Dkt Budemu.

Katika uzinduzi wa matibabu ya upasuaji wa Kibingwa pia imehudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa,Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Seif Kallaghe,Mstahki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shilloo,Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Jonathan Budemu na viongozi wa CCM.

Mwisho.




























Post a Comment

0 Comments