Ticker

6/recent/ticker-posts

ACT WAZALENDO CHAISHUKURU SERIKALI KUTEKELEZA MAPENDEKEZO YAO



**********************

Na Magrethy Katengu

Chama Cha ACT WAZALENDO kimeishukuru Serikali kwa kutekeleza baadhi ya mapendekezo yao kwa wananchi ikiwemo kupunguza bei ya mafuta, kushughukikia Mafao ya wastaafu,kutoa tozo ya miamala ya kifedha ya simu na kibenki, kutoa elimu juu ya uwelewa wa bima ya Afya ili kusaidia kupunguza makali ya maisha magumu kwa wananchi.

Akizungumza leo Jijini Dar es saalam na Waandishi wa habari Waziri Mkuu kivuli wa Chama Cha ACT Wazalendo Dorothy Semu amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassani imekuwa sikifu kusikiliza maoni na mapendekezo ambayo wamekuwa wakiyato mara kwa mara kupitia Wizara zao vivuli hivyo mwaka 2022 unaisha wakiwa na matumaini baadhi ya mapendekezo ambayo hajatekelezwa yatakekelezwa

Waziri Mkuu Kivuli wa ACT Wazalendo Dorothy amesema hivi karibuni walishuhudia kampuni ya kupakua makintena bandarini TITC ikifanya kazi ndivyo sivyo baada ya kutoa mapendezo yao Serikali ilivyomaliza nayo Mkataba imeiachisha kufanya kazi hiyo hivyo wanaiona Serikali ikiwa sikivu kushughukikia maoni na changamoto..

"Katika kipindi cha mwaka 2022 tumetoa matamko 90 mikutano na Waandishi wa habari 31 ziara katika Mikoa 7 hii na kuchambua bajeti ya serikali 2022/2023 pia na kuchambua ripoti ya Mkaguzi wa hesabu za serikali CAG huku tukitoa maoni yetu wapi serikali ifanye marekebisho katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya Ardhi"amesema Semu

Aidha ACT Wazalendo ni chama ambacho kinaaminika hivyo hakiwezi kuona maombo yanaenda ndivyo sivyo kikakaa kimya mwaka 2022 tunaumaliza nchi ikiwa na Amani na Utulivu tutaendelea kutoa Ushirikiano mwaka 2023 kwa kuishauri serikali na kutoa maoni

Post a Comment

0 Comments