Ticker

6/recent/ticker-posts

MACHINGA KINONDONI WAIANGUKIA SERIKALI KUINGILIA KATI WAFANYABIASHARA WANAOJIMILIKISHA MEZA ZAIDI YA MOJA********************

Na Magrethy Katengu

Wafanyabiashara ndogo ndogo (MACHINGA) Wilaya ya Kinondoni waiomba Serikali kuingilia kati kitendo kinachofanywa na baadhi ya Wafanyabiashara wakubwa kuhodhi eneo zaidi ya moja huku wao wakikosa eneo hata la kuweka meza kufanya biashara hivyo kusababisha kuvizia jioni kufanya shughuli zao maeneo yaliozuiwa.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Machinga Wilaya ya Kinondoni Abdalah Mwakilimo amesema Wanashukuru serikali kuwapa utaratibu wa maeneo ya kufanyia shughuli zao lakini changamoto kubwa ni baadhi ya watu ambao hawana huruma kujimilikisha eneo kubwa kinyume na utaratibu na uongozi wa Sokoni ukiwafuata huwa wakaidi kutokana nyuma yao kuna watu kutoka idara ya biashara halmashauri katika halmashauri hiyo.

"Nimechaguliwa kuwa kiongozi kutetea Machinga Wilaya hii ya Kinondoni lakini napitia wakati mgumu sana Machinga wenzangu kunilalamikia wa suala la kukosa maeneo ya biashara huku wakiona baadhi ya wenzao kumikiki eneo kubwa hivyo utakuta mtu mmoja ameweka biashara zake katika eneo moja meza zaidi ya tisa akiwa ameyaandikisha majina ya watoto wake hivyo nikimfuata najibiwa vibaya na kutishiwa naomba ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri tusaidiane kutatua changamoto hii"amesema Abdalah

Aidha Mwenyekiti huyo amesema kuwa Serikali imetoa utaratibu wa Machinga kulingana na mitaji yao ikiamini kuwa atakuwa akifanya shughuli zake huku akitoka hatua moja kwenda nyingine hadi kufikia kuwa mfanyabiashara mkubwa lakini watu wasio na huruma ubinafsi ukiwa umewajaa mioyoni mwao hujimilikisha eneo kubwa huku wenzao wakikosa pa kuweka biashara zao hususani Makumbusho tatizo hili limekuwa sugu .

Sambamba na hayo amesema Machinga ni kundi linalotegemewa na familia zao ikiwemo watoto baba na mama hivyo wakikosa maeneo ya kufanya shughuli zake Ili wajipatie kipato Ili kukidhi mahitaji yao itasababisha kundi kubwa lililopo nyuma yao kuishi maisha magumu wakati mwingine watoto kukosa shule hivyo Serikali iangalie hao wanaohodhi maeneo makubwa na wenzao kukosa maeneo wachukuliwe hatua stahiki ...

Kwa upande wake Msemaji wa Machinga Wilaya ya Kinondoni Sharifu Hassan ameiomba Mamlaka ya Serikali kumpa nguvu Mwenyekiti kwani Masokoni humo kuna Ufisadi Mkubwa sana unaotendeka na watu wachache kujilikisha eneo kubwa ukiangalia hadhi yao siyo ya kuwa Machinga ila wanatumia mwamvuli huo kuwaimiza

"Naishauri Serikali ni vyema maeneo ya biashara yanapogawiwa wawepo kwani kisheria Machinga anatakiwa amiliki meza Moja akimiliki zaidi ya moja si Machinga tena atoke akapange fremu kwani machinga tupo wengi hivyo hata Serikali ikiamua kufanya ukaguzi sisi hatuogopi tutawataja wote wanaomiliki meza zaidi ya moja hatuogopi tumechoka kuona wenzetu wakifanya biashara Barabarani kwa kuvizia usiku maeneo yaliyokatazwa hususani majira ya usiku"amesema Hassani

Naye Mfanyabiashara wa Makumbusho Sokoni Ally Dauda amesema hao amesema wanaomiliki maeneo makubwa hufanya udanganyifu wakati wa kuandikisha wengine huandika majina ya baba zao watoto zao ambao hata umri wa miaka 18 hawajatimiza ambapo ni kinyume na utaratibu

Aidha Machinga wa Wilaya hiyo Wanashukuru Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kuwatambua kuwa wao ni kundi Maalumu hivyo wako chini ya Wizara Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto Wanawake na Makundi Maalumu hivyo nao wanahitajika kupewa huduma na Serikali kitendo alichofanya Rais na imesaidia taasisi za kifenda ikiwemo benki ya Maendeleo benki,NMB kuweza kuwaamini na kuwapatia mikopo Ili wafanye shughuli zao

Pia wameiomba serikalini katika mwaka ujao wa 2023 Soko la Bunju litengenezewe miundombinu daladala,bajaji,pikipiki ziweze kuingia na kutoka Ili kusaidia soko hilo kuchangamka na Machinga wasiache meza zao na kuanza kutembeza bidhaa mitaani

Post a Comment

0 Comments