Ticker

6/recent/ticker-posts

HATUA ZA UTENGENEZAJI BWAWA LA MWALIMU NYERERE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na wananchi wa Mikoa ya Pwani na Morogoro kabla ya kuzindua Shughuli ya Kufunga Njia ya Kuchepusha Maji na Kuanza Ujazaji wa Maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme (Megawati 2115) la Julius Nyerere (JNHPP) kwenye Mto Rufiji Mkoani Pwani tarehe 22 Desemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuashiria Hatua ya Kufunga Njia ya Kuchepusha Maji na Kuanza Ujazaji wa Maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme (Megawati 2115) la Julius Nyerere JNHPP kwenye Mto Rufiji Mkoani Pwani tarehe 22 Desemba, 2022.

****************************

Na Magrethy Katengu..

Hatua ya kwanza, ni kuchoronga na kujenga njia ya kuchepusha maji ya mto ili ili kupata eneo kavu katikati ya mto ili kuweza kujenga tuta kubwa litakalohifadhi maji.

Hatua ya pili, ni kujenga tuta kuu la kuhifadhi maji.

Hatua ya tatu, ni kuchoronga na kujenga njia za kuporomosha maji ili yaweze kuzungusha vinu vya kufua umeme.

Hatua ya nne ni kujenga, kuunga na kusimika mitambo na vinu vya kufua umeme.

Hatua ya tano ni kujenga kituo cha kusafirisha umeme ili uweze kutumika katika gridi ya taifa.

Hatua ya sita ni ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka bwawa la Nyerere mpaka Chalinze ili kuingiza umeme kwenye gridi ya Taifa na kutumiwa na wananchi.

Hatua ya saba ni ujenzi wa daraja la kudumu.

Hatua ya nane ni ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa mradi na barabara za ndani ya mradi.

“Sote katika umoja wetu tunapaswa kujivunia na kudhihirisha umoja, utaifa na uzalendo wetu, kwa kuendeleza na kuulinda mradi huu muhimu kwa maendeleo yetu. Na kwa muktadha huo nazidi kuwakumbusha kuwa mradi huu ni fahari ya nchi yetu na tunautekeleza kwa gharama kubwa na kwa jasho la kila Mtanzania kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vizazi vijavyo” Rais Dkt Samia Suluhu

Post a Comment

0 Comments