Ticker

6/recent/ticker-posts

MABALOZI WANAOWAKILISHA NCHI SEHEMU MBALIMBALI WAMETAKIWA KUHAMASISHA MATUMIZI LUGHA YA KISWAHILI.


Na Zena Mohamed,Dodoma.

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.James Mdoe amewataka mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania sehemu mbalimbali duniani kuongeza kasi ya kuhamasisha zaidi matumizi ya kishwahili hali itakayosaidia lugha hiyo kutambuliwa na watu wengi zaidi.

Amesema hadi sasa watu takribani milioni 250 Dunia wanazungumza kiswahili hii ni kutokana na kukuza lugha ya kiswahili ilikuimarisha hali ya kidiplomasia, uchumi,kujenga amani, maendeleo na utangamano katika kona mbali mbali za dunia.

Hayo yameelezwa leo November 3,2022 Jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.James Mdoe wakati akizindua sherehe za miaka 61 ya uhuru kwenye eneo la utambuzi wa lugha ya kiswahili ambayo itahusisha mashujaa wa lugha hiyo kupandisha bango lenye ujumbe wa kiswahili kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro.

Prof.Mdoe ametaja kauli mbiu ya maadhimisho hayo ya utambuzi wa lugha ya kiswahili kuwa ni,"kiswahili Kileleni"

Aidha Prof.Mdoe ameeleza kuwa Serikali ina mpango zaidi wa kuendeleza makubaliano na vyuo vingine nje ya nchi namna ya kufundisha kiswahili na kuongeza hamasa zaidi kwa watumiaji wa lugha hiyo adhimu.

"Idadi hii inaonesha wazi ni kiasi gani kiswahili kinapendwa na idadi kubwa ya vyuo vikuu 150 ulimwenguni vinatoa mafunzo ya lugha hiyo huku vituo vya radio na television 300 vikiwa vinarusha vipindi kwa lugha ya kiswahili,"amesema.

Kwa upande wake mtaalamu wa lugha ya kiswahili na Mwandishi wa vitabu Kwa lugha kutoka nchini Misri Mina Yasri amesema watanzania wanatakiwa kujivunia lugha yao na kuwataka kutambua kuwa uhuru wa mwafrika upo kwenye lugha yake ya asili na kusisitiza kuwa kuongea kiingereza siyo kuona ndio ustaarabu.

Mwandishi huyo vitabu ameeleza kuwa yeye ndiye Mwandishi wa kwanza nchini Misri kuandika kitabu cha kwanza cha maudhui ya kiswahili hivyo kuwataka watanzania kuwa na ari ya kuzungumza lugha yao ya asili bila kukuonea haya kiswahili.

Hivyo Yasri ametumia nafasi hiyo kuwaomba Viongozi wa ngazi mbalimbali nchini kutumia fursa wanaposafiri kwenye mataifa mengine kukieneza kiswahili na kusisitiza kuwa uongozi bora hupendeza ikiwa kiongozi atapendelea kutumia lugha yake mama.

"Ili mtu aheshimike na wengine anatakiwa kuwa na utambulisho wa pekee wa lugha ya asili na kwamba huo ndiyo ustaarabu na si vinginevyo kwani kujua lugha ya asili ni burudani na uwekezaji na uwajibikaji,"amesema.

Vilevile ameeleza hali ya kiswahili Cairo-Misri eneo anakotoka Mwandishi huyo amesema lugha hiyo tayari inatambuliwa na kuenziwa na watu wengi na kwamba juhudi kidogo bado zinahitajika ili kuongeza nguvu zaidi katika kutafsiri vitabu vya kiarabu kwenda kwenye kiswahili.

"Tunahitaji zaidi kuongeza nguvu katika tafsiri za kiarabu kuwa kiswahili,tafsiri nyingi ni za kiswahili kwenda kiarabu,tunahitaji nguvu kubwa kila mmoja ajue umuhimu wa kiswahili,tunatakiwa kuunganishwa kwa lugha hii,"amesema

Naye mwanamashairi wa lugha ya kiswahili kutoka chuo cha jeshi Kunduchi Mwanakombo Mwanakombo amekielezea kiswahili kama bidhaa inayojiuza na kuuzika duniani kote.

Amesema iwapo lugha hiyo itabidhaishwa vizuri itaendelea kusimamisha uhuru,heshima na umoja na kwamba kwa kuliona hilo lugha ya kiswahili kuadhimishwa kimataifa kila tarehe 7 Julai Kutokana na

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2021 lilitangaza rasmi tarehe hiyo kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.



Post a Comment

0 Comments