Ticker

6/recent/ticker-posts

MASHINDANO YA BULYANHULU HEALTHY LIFESTYLE MARATHON YAVUTIA WENGI


Meneja Mkuu wa Mgodi wa wa Bulyanhulu, Cheick Sangare akiongea katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa wa Bulyanhulu, Cheick Sangare akiongea katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya, akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa wa Bulyanhulu, Cheick Sangare, akikabidhi zawadi ya baiskeli kwa mshindi wa mbio ndefu Elias Charles.
Mtaalamu wa Afya wa Mgodi wa Bulyanhulu,Dk. Nolask Kigodi akiongea katika hafla hiyo (kulia) ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa wa Bulyanhulu, Cheick Sangare.
Baadhi ya washiriki baada ya kumaliza mbio hizo
Baadhi ya washiriki baada ya kumaliza mbio hizo
Baadhi ya washiriki wa mbio hizo wakikimbia kuwania ushindi
Baadhi ya washiriki wa mbio hizo wakikimbia kuwania ushindi
Baadhi ya washiriki wa mbio hizo wakikimbia kuwania ushindi
**

Mashindano ya mbio ya kilomita 42 ya Bulyanhulu Healthy Lifestyle Marathon yaliyoandaliwa na Mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu yamefanyika jana ambapo Elias Charles, ameibuka mshindi wa jumla wa mbio ndefu na kujishindia zawadi ya baiskeli ya kisasa ya kupanda milima aina ya La Ruta 29+.

Mashindano hayo ya mbio zenye urefu wa aina mbalimbali yamewashirikisha washiriki zaidi ya 250 ambao ni wafanyakazi wa Mgodi, wakandarasi wa Mgodi na wananchi wanaoishi kwenye vitongoji vinavyozunguka Mgodi.

Zawadi nyingine ambazo wamejinyakulia washindi katika mbio za Kilometa 21, 15, 10 na 5, ni pamoja na jokofu, simu janja, saa ya kisasa, mikeka ya mazoezi ya yoga na mashine za kutengeneza salasi na kukamua juisi.

Mgeni rasmi katika hafla alikuwa ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya, ambaye pamoja na kuwapongeza washiriki hao alisema kuwa ofisi yake itashirikiana na Mgodi katika kuhakikisha watumishi na wakandarasi wake wanapata miongozo ya lishe ya taifa ambayo kwa sasa imeanza kutumika katika ngazi zote kuanzia Serikali kuu hadi kwenye kata na vijiji. "Unene na kasi ya magonjwa yatokanayo na mifumo ya maisha yanaongezaka hivyo Serikali imeamua kulivalia njuga changamoto hii".

Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Mgodi wa wa Bulyanhulu, Cheick Sangare, alisema kuwa kampuni imejipanga kuhakikisha kuwa suala la afya za wafanyakazi inalipa kipaumbele kwa kuwa inaamini kuwa kuwa na nguvu kazi yenye afya bora kunaleta tija zaidi.


Naye mtaalamu wa afya kutoka Mgodi huo, Dk. Nolask Kigodi, alisema mgodi ulikuwa na lengo la kupunguza uzito wa jumla wa kilo 1,500 kwa wafanyakazi wapatao 2,500 ikiwemo wakandarasi mbalimbali waliopo mgodini hapo. “Tumejipanga kuhakikisha suala la mazoezi linapewa kipaumbele sambamba na kuwa na sehemu za kufanyia mazoezi zenye vifaa mbalimbali na kuzingatia lishe bora.


Post a Comment

0 Comments