Ticker

6/recent/ticker-posts

MAFUNZO KWA WAVUVI YAHITIMISHWA RASMI KI MKOA.

Matukio katika kufunga mafunzo kwa wavuvi wilaya Muleba , katikati ni mhe Toba Nguvila katibu tawala mkoa na bi Kemilembe Rwota kaimu Mkuu wa Wilaya Muleba .


*********************

Na Shemsa Mussa.

Mafunzo hayo yaliyofanyika siku 7 ndani ya mkoa kagera yamehitimishwa leo jumapili Desember 4 na katibu tawala wa Mkoa mhe, Toba Nguvila kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa mhe, Albert Chalamila,Mafunzo hayo yamehitimishwa katika wilaya ya muleba kwa wananchi wa mwalo wa Magarini ndani ya kata Nyakabango .

Akizungumza na wananchi hasa wavuvi mhe Toba Nguvila amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kwa ajili ya kujiokoa wao pamoja na kuwaokoa wengine endapo tatizo likitokea na kuwasihi wavuvi hao kuendelea kufanya mazoezi na kuwafundisha wengine .

‘’Nawasisitiza endeleeni kufanya mazoezi kwa kile mlichojifunza na muwafundishe wengine ili wageni na wenyeji wajue zaidi na nawaambia hivyo vifaa mlivyopewa kama life jaket msizivue mkiwa Ziwani kwa kuhisi joto huwezi kujua baada ya kuvua nini kitatokea kwa muda huo, Alisema Nguvila’’

Pia mh Nguvila amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Muleba kutenga fedha kwa ajili ya kufanya mwendelezo wa Mafunzo kwa wavuvi .

‘’ikiwa asilimia kubwa ya mapato ya wilaya yanatokana na uvuvi sioni kama ni jambo la kushangaza kutenga fedha kwa ajili ya kuwapa mafunzo zaidi wavuvi ambao ni tegemeo la wilaya katika uchumi ,tenga fedha kila baada ya miezi 6 wanapata mafunzo ambayo yataambatana na kupinga uvuvi haramu, Amesema Nguvila’’

Nae Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha Maafa bw Prudence Kostantine amesema kuwa mafunzo hayo yalianza lasmi Nevember 28 ndani ya Mkoa Kagera wameweza kukutana na wavuvi katika maeneo ya wilaya za Bukoba 50,Misenyi 10 , muleba na baadhi ya visiwa vya Kerebe 79 ,Gozba 38 ,Mazinga 35 na Bumbile 77 ,ikiwa nchi kavu ni 55 jumla ya wavuvi wote wailopata mafunzo wakiwa 344. Na kusema kuwa baada ya mkoa kagera watapanga ni mkoa upi unafuata kwa muda mfupi na lengo ni kuwapa mafunzo wavuvi wote wanaopakana Ziwa na Bahari Ndani ya nchi.

Post a Comment

0 Comments