Ticker

6/recent/ticker-posts

MOEST NA WMU ZAUNGANA KUZINDUA KAMPENI YA KISWAHILI/TUKUTANE KILELENI


Na Mwandishi Wetu,

5.12.2022

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii imezindua Kampeni ya TUKUTANE KILELENI ikiwa ni shamrashamra za kusheherekea miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

Kampeni hiyo yenye lengo la kuhamasisha Watanzania kupanda Mlima Kilimanjaro imezinduliwa Jumamosi Desemba 3 mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana.

Ushiriki huo wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika kampeni hiyo pia umelenga kuitangaza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya mipaka kwa kusimika bango la Wizara lenye kubeba kauli mbiu isemayo KISWAHLI KILELENI katika kilele cha Mlima Kilimanjaro siku ya tarehe 9 Desemba, 2022.

Akizungumza katika Hafla hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana amesema hatua hiyo ya kuunganisha wadau wa utalii ziikiwemo zikiwemo Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ni hatua mojawapo ya kutekeleza kwa vitendo ziara ya Mhe. Rais Samia Suluh Hassan alieongoza uzinduzi wa filamu ya Royol tour katika kuhimiza utalii wa ndani.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamini Sedoyeka aliishukuru Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kubuni kampeni hiyo ya kuitangaza lugha ya Kiswahili kwani itaweza kuvutia watalii wengi Zaidi kujifunza lugha hiyo wakiwa nchini.

Katika kampeni hiyo, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inawakilishwa na Bi. Hilda N. Bukozo, ambaye ni Mratibu Mkuu wa Kielimu Kikanda na Kimataifa akiandamana na wapanda Mlima wawili Bw. Suleiman Omary Chamshama na Bw. Nestory Thobas Owano pamoja na wanahabari na Mratibu wa Kiswahili wa Wizara Dkt. Maryam Mwinyi.

Wapanda Mlima hawa wanatarajiwa kurejea siku ya tarehe 9 Desemba mwaka huu ambayo ni siku ya maadhimisho ya Kitaifa.

Post a Comment

0 Comments