Ticker

6/recent/ticker-posts

MUTAFUNGWA APIGA MARUFUKU DISKO TOTO
************************

Na Sheila Katikula, Mwanza

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza,Wilbroad Mutafungwa amewataka wazazi na walezi kuacha kuwapeleka watoto wao kwenye disko toto kipindi cha sikukuu za christmas na mwaka mpya.

Wito huo ametolewa leo wakati akizungumza na Waandishi ofisini kwake na kueleza kuwa kila mazazi na malezi anaowajibu wa kumlinda watoto ili waseinde kwenye disko toto ambapo wanaweza kupata matatizo .

"Hatutaki kuona kitu kinaitwa disko toto mkoani kwetu tunaomba wazazi watusaidie kuhakikisha watoto wahawaendi katika mikusanyiko hiyo ambayo hata leseni za biashara hazijatolewa na mamlaka zinazohusika kwenye maeneo hayo na kupelekea msongamano usiyokuwa ya lazima ambao unaweza kuleta madhara kwa afya za watoto hao.

Amewataka wazazi na walezi kuacha na tabia ya uzembe ya kumwamini kila mtu na kumwachia mtoto kwani wanapaswa kuwa makini na watoto wao.

Hata hivyo ameongeza kuwa suala la ulinzi na usalama siyo la vyombo vya usalama peke yake bali kila mtu anawajibu wa kuchukua tahadhali ili kuweza kusherehekea sikukuu hizo kwa amani.

Amesema kuna baadhi ya watu husherehekea sikukuu hizo kwa kuchoma mataili,kuendesha pikipiki kwa fujo na kupelekea taharuki kwa wananchi ambao wanautumia barabara hizo kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria pia ni vitendo ambavyo vinaweza kuchochea uvunjifu wa amani.

"Hatuta kubali kuona barabara zetu zinachafuliwa na watu ambao wanataka kumaliza mwaka kwa kuchoma mataili wakae wakijua lokapu zetu zinawasubili kwani tumeweka polisi kila kona ikiwemo makanisani na barabarani ili waweze kuwakamata watu wanaofanya uhalifu ",amesema Mutafungwa.

Hata hivyo amewataka wananchi kuendelea kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili ziweze kufanyiwa kazi kwani jeshi hilo lipo imara kuhakikisha linawalinda watu wote ili waweze kuishi kwa amani na utulivu.

Post a Comment

0 Comments