Ticker

6/recent/ticker-posts

WADAU WA MAENDELEO KANYIGO WAUNG'ARISHA USHARIKA WA KIGARAMA.*************


Na Shemsa Mussa, Kagera

Wadau wa maendeleo katika kata ya kanyigo wilaya Missenyi wamechanga kiasi cha shiling Milioni 64 ikiwa ni jitihada za kuendeleza miundombinu ya kanisa la kigarama pamoja na kabambiro.

Wadau hao wameweza kuchangia kiasi hicho cha fedha katika siku ya kigarama parishi ambayo imezinduliwa leo kwa ajili ya kusimika na kuendeleza maendeleo ya usharika huo wa dayosisi ya kaskazini Magharibi Jimbo la kaskazini A: usharika wa kigarama .

Akizungumza mbele ya Mgeni Rasimi katika hafla hiyo Mchungaji wa kanisa hilo Bw Samwel Rwezaula amesema kuwa fedha hizo zimechangwa na kutoka kwa waumini , wazawa wa kanyigo pamoja na wadau wa maendeleo kwa lengo la ujenzi wa na ukarabati wa vyoo katika kanisa zote mbili pa moja na ukarabati wa kanisa la kigarama.

"Tumejenga choo kipya cha hapa kigarama lakini tumekarabati choo cha zamani cha kabambiloa na tumekarabati kanisa la kigarama na shughuli nyingine zinaendelea "amesema Mchungaji"

Nae Baba askofu Abernego Keshomshahara ambaye alikuwa mgeni rasimi amesema kuwa ni vema miundominu inayojengwa itunzwe na kuhifadhiwa kwa uchungu na umakini zaidi na kigarama iwe sehemu ya kuigwa katika kuleta maendeleo .

"Kigarama iwe sehemu ya kujifunza kwa maendeleo na nawasisitiza washarikra/waumini kutunza miundombinu inayojengwa na bahati nzuri naona ujenzi wa choo na wakisasa kwa hiyo sitegemei kukuta matundu yamezibwa kwa makuti ya migomba "amesema Baba Askofu Keshomshahara".

Nae Mbunge wa jimbo hilo Mhe Frorence Kyombo ambaye alikuwa moja ya wageni waalikwa amesema kuwa serikali ya Rais Samia Suluhu Hassani inania ya kuendeleza miradi mbalimbali ndani ya wilaya missenyi ikiwemo barabara,zahanati, pamoja na uboreshaji wa vituo vya Afya zaidi , hivyo amewasihi wananchi kuwa na subra na matumaini na serikali yao.


Post a Comment

0 Comments