Ticker

6/recent/ticker-posts

TAMASHA KUBWA LA UIMBAJI NA UPONYAJI KUBADISHA WATU KUOKOLEWA KUTOKA VIFUNGO VYA SHETANI*******************

Na Magrethy Katengu

Mwinjilisti wa kimataifa kutoka nchini Canada Dkt Peter Youngreen amekuja kufanya Mahubiri makubwa katika Tamasha kubwa la Uimbaji na uponyaji kuanza leo saa tisa alasiri katika kanisa la BCIC Mbezi Beach Jogoo Dar es salaam linaloongozwa na Askofu Sylvester Gamanywa huku miujiza mikubwa na uponyaji .

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam mwenyeji wa tamasha hilo Askofu Sylvester Gamanywa amesema kuwa tamasha hilo litakuwa la kipekee kabisa haijawahi kutokea hivyo Mungu atadhihirika kwa watu wake mwezi huu Desemba waliokata tamaa kiuchumi,kiafya,kisiasa watapokea miujiza kupitia maombi yatakayofanyika

" Tanzania imepata neema kubwa ya kutembelewa na mhubiri huyo wa kimataifa na itapokea baraka na miujiza hivyo watu wote wanakaribishwa hatubagui dini lugha wala kabila Mungu ni wa wote" amesema Askofu.

Kwa upande wake muinjilisti huyo wa kimataifa Dkt Peter Youngreen ameishukuru kwa mapokezi aliyoyapata hapa nchini na kusisitiza kuwa kupitia tamasha hilo watanzania watamwona Mungu kupitia Uimbaji Mahubiri maombi hivyo waje Yesu Kristo aliyekufa kwa ajili ya wote anawaita.

"Utajiri mkubwa kuliko wote duniani ni watu hivyo watu wanapaswa kumjua mwenyezi Mungu Ili kwani ndiye aliyeumba Dunia na vyote vilivyomo hivyo uhai walio nao wamepewa bure "amesema Dkt Peter

"Nataka kuongea na Afrika na wakati huu wa kufunga mwaka nataka niwaambie vijana wa bara hili wamtambue Yesu Kristo kuwa nyakati tulizonazo sasa katika dunia siyo njema hivyo kama vijana watamjua Yesu Kristo na kumuamini watapokea miujiza wao na Taifa Kwa ujumla "amesema mwinjilisti huyo wa kimataifa

Hata hivyo amesema wakati akipanga safari yake kuja Tanzania alionyeshwa maino na Mungu watu wengi waliokata tamaa lakini baadaye kupitia neno la Mungu wakapokea miujiza hivyo anawakaribisha sana watu wote hapa Wapo Mission Center waje kupokea miujiza walemavu viwete wenye mapepo wasio na ajira waliokata tamaa Yesu Kristo atabadili Maisha yao

Post a Comment

0 Comments